Posted By Posted On

ARSENAL MABINGWA WA NGAO YA JAMII ULAYA,WAINYOOSHA LIVERPOOL, on August 29, 2020 at 6:10 pm

 Arsenal leo Agosti 29 imetwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kushinda kwa mikwaju 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.Mchezo wa leo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa msimu wa 2020/21.Pierre Emerick Aubameyang alianza kufunga dakika ya 12 kwa Arsenal kisha Takumi Minamino aliweka usawa dakika ya 73.Jitihada za Liverpool kusaka taji la kwanza kwa msimu wa 2020/21 zimegonga mwamba baada ya kufungwa kwa penalti.Licha ya Liverpool kupiga mpira mwingi wakimiliki asilimia 60 huku Arsenal 40 na kwa upande wa mashuti walikipiga jumla ya mashuti 15 huku Arsenal ikipiga mashuti 8.Yaliyolenga lango kwa Liverpool ni mashuti 4 huku Arsenal yakilenga mashuti 2 waliambulia patupu Uwanja wa Wembley.,

 

Arsenal leo Agosti 29 imetwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kushinda kwa mikwaju 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Mchezo wa leo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu England kwa msimu wa 2020/21.

Pierre Emerick Aubameyang alianza kufunga dakika ya 12 kwa Arsenal kisha Takumi Minamino aliweka usawa dakika ya 73.

Jitihada za Liverpool kusaka taji la kwanza kwa msimu wa 2020/21 zimegonga mwamba baada ya kufungwa kwa penalti.

Licha ya Liverpool kupiga mpira mwingi wakimiliki asilimia 60 huku Arsenal 40 na kwa upande wa mashuti walikipiga jumla ya mashuti 15 huku Arsenal ikipiga mashuti 8.

Yaliyolenga lango kwa Liverpool ni mashuti 4 huku Arsenal yakilenga mashuti 2 waliambulia patupu Uwanja wa Wembley.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *