HUYO STRAIKA MPYA YANGA UTAMPENDA TU, on August 12, 2020 at 7:57 am

NA WINFRIDA MTOI YANGA imeendelea kushusha vifaa vipya, safari hii imetambulisha jembe la kimataifa kutoka Burkina Faso, Songne Yacouba, aliyekuwa akikipiga kwenye klabu kogwe ya Asante Kotoko ya Ghana. Kutokana na sifa zinazotolewa na wachezaji wenzake wanaoifahamu kazi yake uwanjani, ni lazima shabiki yoyote wa Yanga atampenda tu. Straika huyo aliyesaini kandarasi ya miaka miwili
The post HUYO STRAIKA MPYA YANGA UTAMPENDA TU appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI


YANGA imeendelea kushusha vifaa vipya, safari hii imetambulisha jembe la kimataifa kutoka Burkina Faso, Songne Yacouba, aliyekuwa akikipiga kwenye klabu kogwe ya Asante Kotoko ya Ghana.
Kutokana na sifa zinazotolewa na wachezaji wenzake wanaoifahamu kazi yake uwanjani, ni lazima shabiki yoyote wa Yanga atampenda tu.
Straika huyo aliyesaini kandarasi ya miaka miwili Jangwani, aliwahi kuwahenyesha Simba katika mechi ya tamasha la Simba Day mwaka 2018, mechi iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mpaka, Dar es Salaam.
Yanga ilimtambulisha mchezaji huyo jana na anatarajia kutua nchini muda wowote kuanzia sasa.
Songne amejiunga na Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba Asante Kotoko Aprili Mosi, mwaka huu.
Mchezaji huyo ambaye pia alikuwa akifukuziwa na Orlando Pirates inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini, alijiunga na Kotoko mwaka 2018.
Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga iliyoweka katika mitandao ya klabu hiyo, imethibitisha kumsajili nyota huyo.
Mchezaji huyo kupitia video iliyowekwa na Yanga, alisema amefurahi kujiunga na timu hiyo na kuwashukuru viongozi na wataalamu wa Yanga waliofanikisha dili hilo.
“Natarajia kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, naamini timu hiyo itakuwa ni njia ya kufikia mafanikio, ninatarajia kuungana na timu muda si mrefu, nawashukuru viongozi wataalamu wa Yanga,” alisema Yacouba.
DIMBA Jumatano limezungumza na mchezaji wa zamani wa Azam FC, Yahya Mohammed, ambaye anamfahamu vizuri nyota huyo na kusema Yanga imepata mtu.
Mohammed ambaye wamecheza pamoja na mchezaji huyo katika Ligi Kuu Ghana alisema, Songne ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, pia yuko fiti kimwili, hawezi kusumbuliwa na mabeki.
“Yacouba ni mchezaji mwenye kila kitu anachotakiwa kuwa nacho straika, Asante Kotoko tu wenyewe hawakuwa ‘serious’, hadi wamemuachia na alikuwa akitakiwa na timu nyingi hapa Ghana,” alisema.
Alieleza kuwa timu nyingi za Ghana hazina fedha ya kumlipa kwa sababu ni mchezaji ghali na mzuri anayemvutia kila mtu.
“Hajafunga mabao mengi, lakini ni mzuri akiwa na mpira na anatengeneza nafasi za kumfanya mtu mwingine afunge kirahisi na yeye ni mfungaji pia.
“Ubora wake ni zaidi ya Morrison, muhimu ni kumfanya awe na furaha na kumpa kile walichokubaliana, hapo watafurahi wenyewe uwanjani, naamini ataisaidia Yanga sana,” alisema.
Aidha Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Hersi Said, alisema bado wanaendelea kuboresha kikosi hicho na watakuwa wanamtangaza kila mchezaji waliyemalizana naye.
“Kama tulivyofanya kwa wachezaji wote tuliowasajili, tutaendelea kumtambulisha kila mmoja, tumeanza na wakimataifa kama tulivyoahidi kwa Wanayanga na waendelee kuwa watulivu,” alisema.
Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza namba zote za mbele, awali alikuwa akihusishwa kutua Simba ambayo aliwahi kucheza nayo akiwa Asante Kotoko katika mechi ya tamasha la Simba Day, Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Usajili huo unakuwa wa kwanza wa kimataifa kwa Yanga, unafikisha jumla ya wachezaji sita wapya, huku Wanajangwani hao wakimuongezea mkataba wa miaka minne kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Wachezaji wengine wapya waliotua Jangwani ni Bakari Mwamnyeto ‘Nondo’ (Coasta Union), Yassin Mustapha (Polisi Tanzania), Wazir Junior (Mbao FC), Zawadi Mauya (Kagera Sugar) na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (mcheaji huru).

The post HUYO STRAIKA MPYA YANGA UTAMPENDA TU appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *