Posted By Posted On

JKT TANZANIA IPO KAMILI GADO KWA MSIMU WA 2020/21, on August 29, 2020 at 1:55 pm

 UONGOZI wa JKT Tanzania umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya msimu wa 2020/21 kwa kuwa kikosi kipo kamili kwa ajili ya kupambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea.Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa maandalizi kwa sasa yameanza kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza Septemba 6.”Kila kitu kipo sawa tumejipanga kuona kwamba mashabiki wanapata burudani na mpira wa kitabuni kwani falsafa yetu inajulikana kwa muda mrefu ni tangu msimu uliopita tumekuwa tukitoa burudani.”Wachezaji wapo kambini na hatuna mpango wa kusajili wachezaji wengi kwani hakuna muda mrefu kwa ajili ya maandalizi kwa msimu mpya hivyo benchi la ufundi limependekeza tubaki na nyota wengi wa msimu uliopita ili kuwapa muda wa kuendelea kufanya vizuri,” amesema. Katika kujiweka sawa na msimu mpya, JKT Tanzania jana ilicheza mchezo wa kirafiki na Polisi Tanzania na kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.,

 


UONGOZI wa JKT Tanzania umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya msimu wa 2020/21 kwa kuwa kikosi kipo kamili kwa ajili ya kupambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa maandalizi kwa sasa yameanza kwa ajili ya msimu mpya ambao unatarajiwa kuanza Septemba 6.

“Kila kitu kipo sawa tumejipanga kuona kwamba mashabiki wanapata burudani na mpira wa kitabuni kwani falsafa yetu inajulikana kwa muda mrefu ni tangu msimu uliopita tumekuwa tukitoa burudani.

“Wachezaji wapo kambini na hatuna mpango wa kusajili wachezaji wengi kwani hakuna muda mrefu kwa ajili ya maandalizi kwa msimu mpya hivyo benchi la ufundi limependekeza tubaki na nyota wengi wa msimu uliopita ili kuwapa muda wa kuendelea kufanya vizuri,” amesema.

 Katika kujiweka sawa na msimu mpya, JKT Tanzania jana ilicheza mchezo wa kirafiki na Polisi Tanzania na kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *