Kama rekodi zitacheza, basi Lyon hana chake vs Bayern Munich leo, on August 19, 2020 at 10:07 am

LISBON, Ureno NANI kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu? Lyon au Bayern Munich? Klabu hizo ziliingia nusu fainali baada ya kufanya mauaji makali dhidi ya Manchester City na Barcelona kwa kufuatana. Lyon walishinda mabao 3-1 dhidi ya kikosi hicho kinachofundishwa na kocha raia wa Hispania, Pep Guardiola huku Bayern Munich wakiitandika kipigo
The post Kama rekodi zitacheza, basi Lyon hana chake vs Bayern Munich leo appeared first on Gazeti la Dimba.,

LISBON, Ureno

NANI kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu? Lyon au Bayern Munich? Klabu hizo ziliingia nusu fainali baada ya kufanya mauaji makali dhidi ya Manchester City na Barcelona kwa kufuatana.

Lyon walishinda mabao 3-1 dhidi ya kikosi hicho kinachofundishwa na kocha raia wa Hispania, Pep Guardiola huku Bayern Munich wakiitandika kipigo cha mbwa mwizi Barcelona cha mabao 8-2.

Hata hivyo, rekodi za klabu hizo mbili zikikutana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zinaibeba zaidi Bayern Munich ambao wanataka kuandika rekodi ya kubeba mataji matatu msimu huu kwa mara ya pili baada ya kufanya hivyo mwaka 2013.

Lyon na Bayern Munich zimekutana mara tisa katika michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mara ya mwisho zilikutana hatua kama hii msimu wa 2009/10. Wakali hao wa Ujerumani wameshinda mechi tano, sare mbili na kufungwa mara mbili.

Hii itakuwa nusu fainali ya 12 kwa Bayern Munich, wakizidiwa mara moja na Real Madrid (13), lakini, mabingwa hao wa Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, walishindwa kusonga mbele tangu walivyofanya hivyo msimu 2012/13 ambao walitwaa ubingwa wa Ulaya.

Pia, Bayern ni timu ya pili kushinda michezo tisa mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakiwa sawa na Barcelona waliofanya hivyo msimu wa 2002/03. Lakini, Wajerumani haoa watafikia rekodi yao ya kushinda mechi 10 mfululizo sawa na Real Madrid kama watashinda dhidi ya Lyon.

Upande mwingine, Rudi Garcia anayekinoa kikosi cha Lyon atakuwa kocha wa pili raia wa Ufaransa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wa mwisho kufanya hivyo alikuwa Didier Deschamps aliyekuwa na AS Monaco msimu wa 2003/04.

Pia, kiungo wa Lyon, Houssem Aouar ametoa asisti saba katika michezo 14 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, tangu alipoanza kucheza msimu wa 2018/19 huku akizidiwa na Kylian Mbappe (10) na Riyad Mahrez (8).

Naye, straika kinara wa michuano hiyo msimu huu, Robert Lewandowski amefunga katika michezo nane mfululizo, akizidiwa na Ruud van Nisterlooy (9) na Cristiano Ronaldo (11).

Lyon possible XI: Lopes, Marcelo, Denayer, Marcal, Dubois, Caqueret, Guimaraes, Aouar, Cornet, Ekambi, Memphis.

Bayern Munich XI: Neuer, Kimmich, Boateng, Alaba, Davies, Goretzka, Thiago, Gnabry, Muller, Coman, Lewandowski.

The post Kama rekodi zitacheza, basi Lyon hana chake vs Bayern Munich leo appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *