Kaze azingua, Pluijm anukia Yanga,, on August 27, 2020 at 7:52 am

NA ZAINAB IDDY WAKATI mashabiki wakijiandaa kufanya kupokea Cedric Kaze, hali imebadilika baada ya kocha huyo kuachana na mpango wa kujiunga na Wanajangwani hao kwa madai ya kukabiliwa na matatizo ya kifamilia. Hivi karibuni Yanga, ilimtangaza Kaze, raia wa Burudi  kuwa ndiye atakayekuja kuchukua mikoba ya Luc Eymael aliyetimuliwa. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,,

NA ZAINAB IDDY

WAKATI mashabiki wakijiandaa kufanya kupokea Cedric Kaze, hali imebadilika baada ya kocha huyo kuachana na mpango wa kujiunga na Wanajangwani hao kwa madai ya kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Hivi karibuni Yanga, ilimtangaza Kaze, raia wa Burudi  kuwa ndiye atakayekuja kuchukua mikoba ya Luc Eymael aliyetimuliwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, alisema mipango ya Kaze kuja Tanzania Ijumaa ilishakamilika, lakini leo mchana wamepokea taarifa kuwa kocha huyo hatoweza kuwasili siku hiyo.

“Ni taarifa ya kushtua kidogo kwa sababu tulijua tayari suala la kocha mkuu tulishalimaliza baada ya kufanya mazungumzo naye na kukubaliana aje, lakini pia tulishampa kiasi kidogo cha fedha kumuhakikisha kuwa tunamuhitaji.

“Kwa mujibu ya taarifa aliyotutumia leo (jana) mchana, inaeleza ana matatizo ya kifamilia, hivyo hatoweza kufika hiyo Ijumaa tuliyokubaliana na badala yake apewe mezi mmoja au miwili ili amalize matatizo,” alisema.

Said aliongeza: “ Kutokana na hali hiyo, tunalazimika kukutana kwa dharau na Kamati ya Utendaji ya Yanga  kujadiliana juu ya hili lililojitokeza, aidha kumpa hiyo miezi miwili au mmoja alioutaka au kumtafuta kocha mwingin.”

Habari zaidi kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa kutokana na hali iliyojitokeza, ni wazi wazo la kumrejesha kocha wa zamani wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, litafufuliwa kwani ndiye aliyekuwa chaguo namba mbili baada ya Kaze.

“Naiona nafasi ya Pluijm akiwa pamoja na Juma Mwambusi (kocha msaidizi), kwa haraka haraka sidhani kama atapatikana mwingine zaidi yake, ukizingatia awali alikuwa chaguo namba mbili baada ya Kaze,” alisema mtoa habari wetu wa uhakika.

Ikumbukwe Pluijm alishawahi kufanya kazi na Mwambusi Yanga, hivyo ni wazi uwezekano wa Mholanzi huyo kurejea Jangwani, hata kama ni kwa mkataba wa mwaka mmoja, ni mkubwa.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *