Kigogo Yanga aimwagia sifa GSM,, on August 24, 2020 at 8:44 am

NA MWANDISHI WETU MWANACHAMA maarufu wa Yanga, Dk. Athuman Kihamia, amepongeza usajili wa wachezaji wapya uliofanywa na klabu hiyo, chini ya wadhamini wao, Kampuni ya GSM Group. Dk. Kihamia ambaye amewahi kushika nyadhifa kadha wa kadha ndani ya Yanga kwa sasa akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, ameliambia BINGWA kuwa anaamini usajili,

NA MWANDISHI WETU

MWANACHAMA maarufu wa Yanga, Dk. Athuman Kihamia, amepongeza usajili wa wachezaji wapya uliofanywa na klabu hiyo, chini ya wadhamini wao, Kampuni ya GSM Group.

Dk. Kihamia ambaye amewahi kushika nyadhifa kadha wa kadha ndani ya Yanga kwa sasa akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, ameliambia BINGWA kuwa anaamini usajili uliofanywa safari hii, utarejesha heshima ya Yanga.

Alisema kuwa kwa misimu mitatu iliyopita, Yanga imeshindwa kupata wachezaji wa kiwango cha juu kutokana na ubabaishaji uliokuwapo katika kusaka vifaa, hivyo kuwapa wakati mgumu mashabiki.

“Ukiangalia mchezaji kama Tuisila (Kisinda) na Mukoko (Tonombe), wote ni wa kiwango cha juu, wanatokea timu ambayo ni tishio Afrika hivyo wana uzoefu wa kuweza kuisaidia Yanga msimu ujao.

“Lakini pia kuna wachezaji wengine wapya wanakuja, akiwamo kiungo kutoka Angola (Carlos Carlinhos) ambaye anaonekana ni mzuri sana. Nadhani mashabiki na wanachama wa Yanga kilichopo mbele yetu kwa sasa ni kuunga mkono uongozi wa klabu yetu na wadhamini wetu GSM,” alisema. Dk. Kihamia ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi, Kaliua na Manispaa ya Arusha, kabla ya kupewa nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Rombo, alikuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *