Kocha mpya Yanga atua na CV ya Minziro,, on August 24, 2020 at 8:21 am

NA ZAINAB IDDY KOCHA mpya wa Yanga, Kaze Cedrick anatarajiwa kutua nchini leo ya kesho, tayari akiwa ametumiwa wasifu (CV) wa walimu kadhaa ili kuchagua msaidizi wake. Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla, alimtangaza rasmi Cedrick juzi jijini Dodoma kuwa ndiye mrithi Luc Eymael, akipewa mkataba wa miaka miwili. “Suala la benchi la ufundi limeshakamilika,

NA ZAINAB IDDY

KOCHA mpya wa Yanga, Kaze Cedrick anatarajiwa kutua nchini leo ya kesho, tayari akiwa ametumiwa wasifu (CV) wa walimu kadhaa ili kuchagua msaidizi wake.

Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla, alimtangaza rasmi Cedrick juzi jijini Dodoma kuwa ndiye mrithi Luc Eymael, akipewa mkataba wa miaka miwili.

“Suala la benchi la ufundi limeshakamilika baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili na kocha Cedrick raia wa Burundi, lakini pia tumempa nafasi ya kumchagua msaidizi kutoka ndani au nje ya Tanzania, tupo tayari kumleta.

“Jambo zuri Cedrick hana masharti sana kwani amesema yupo tayari kufanya kazi hata na kocha msaidizi kutoka Tanzania, lakini bado tumempa nafasi ya kupitia CV tuliowahi kutamani kufanya nao kazi, kisha atupe jina lake, kabla ya kilele cha Wiki ya Wananchi, tutamuweka wazi,” alisema Msolla.

Japo Msolla hakutaja jina la kocha yeyote ambaye CV yake ipo mikononi mwa Cedrick, lakini BINGWA limedokezwa kuwa yupo beki wa zamani wa kulia wa Yanga, Fred Felix Minziro, lakini pia kocha wa Namungo, Hitimana Thiery.

Cedrick anakuja kufanya kazi akiwa ni mmoja kati ya makocha wachache wenye leseni A za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) hapa Tanzania, lakini pia akiwa na leseni ya Chama cha Soka cha Ujerumani (DFB).

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *