KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA,, on August 28, 2020 at 10:32 am

NA MWANDISHI WETU NIKOLA Kavazovic anapewa nafasi kubwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, akibeba mikoba ya Luc Eymael aliyetimuliwa, BINGWA limetonywa. Kocha huyo aliyezlaiwa Julai 29, 1975, mjini Belgrade, nchini Yugoslavia, akiwa na uraia wa Serbia, amepata zali hilo baada ya Cedric Kaze wa Burundi juzi kughairi kutua nchini kuinoa Yanga kwa madai ya kukabiliwa,

NA MWANDISHI WETU

NIKOLA Kavazovic anapewa nafasi kubwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, akibeba mikoba ya Luc Eymael aliyetimuliwa, BINGWA limetonywa.

Kocha huyo aliyezlaiwa Julai 29, 1975, mjini Belgrade, nchini Yugoslavia, akiwa na uraia wa Serbia, amepata zali hilo baada ya Cedric Kaze wa Burundi juzi kughairi kutua nchini kuinoa Yanga kwa madai ya kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Akizungumza na BINGWA jana, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, alisema kuwa hadi jana mchana, Kavazovic ndiye aliyekuwa amechaguliwa kuinoa timu hiyo.

“Baada ya Cedric Kaze kuchomoa dakika za mwisho, kilifanyika kikazo kizito jana (juzi) usiku na kupitia CV (wasifu) za makocha wote walioomba kazi Yanga, ndipo jina la Nikola likapitishwa.

“Moja ya sababu za Nikola kupewa kazi, ni mafanikio yake aliyoyapata akiwa kocha wa Township Rollers ya Botswana, ikumbukwe kuwa timu hiyo ilitutoa (Yanga) katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nikola akiwa na Township, alifanikiwa kutwaa mataji kibao, ikiwemo kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ambayo timu hiyo ilikuwa haijawahi kuifikia,” alisema.

Alisema kuwa tayari uongozi wa Yanga umeshawasiliana na kocha huyo juzi na kukubaliana naye, akitarajiwa kutua nchini kesho tayari kwa utambulisho katika tamasha la klabu hiyo la Wiki ya Wananchi litakalofanyika keshokutwa.

Kavazovic ni kocha mwenye leseni A ya UEFA, huku akiwa anashikilia rekodi ya kuwa kocha kijana zaidi kuwahi kuinoa timu ya Taifa, akiwa na umri wa miaka 36.

Hii si mara ya kwanza kwa Kavazovic kuhusishwa na Yanga, kwani msimu uliopita kabla ya kutimuliwa kwa Mwinyi Zahera, alitajwa kuwaniwa na wakali hao wa Jangwani.

Mbali ya kuinoa Township Rollers kuanzia msimu wa 2017-2018, Kavazovic pia aliwahi kufanya kazi na Leopards ya Kenya mwaka 2018 na Klabu ya Free State ya Afrika Kusini msimu wa 2018-2019.

Kavazovic anaonekana kulijua vyema soka la Afrika kutokana na uzoefu wake wa kufundisha klabu kadhaa hapa barani humo, hivyo iwapo atatua Yanga, hatakuwa na kazi kubwa kutekeleza majukumu yake.

Hata hivyo, habari zaidi kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa ukiachana na Kavazovic, pia jina la kocha wa zamani wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, naye anapewa nafasi ya kurejea Jangwani.

“Japo Kavazovic ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuja Yanga, lakini huwezi kujua, anaweza akaletwa kocha mwingine kutegelea na hali itakavyokuwa kwani kuna presha kubwa kutoka kwa viongozi wa Serikali ambao ni Yanga wakitaka kocha aletwe haraka.

“Kwa jinsi ainavyoonekana, kuna vigogo wa Yanga waliopo serikalini na wengine waliostaafu ambao wanapigana usiku na mchana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa, ikiwamo suala hilo la kocha,” alisema mtoa habari wetu wa uhakika ambaye ndiye aliyetutonya juu ya ujio wa Carlos Carlinhos wa Angola na BINGWA kuwa gazeti la kwanza kuripoti kuhusiana na kusajiliwa kwake na Wanajangwani hao.

MJUE NIKOLA KAVAZOVIĆ

KUZALIWA:    Julai 29, 1975

MAHALI:         Belgrade, Yugoslavia

Urefu:             M 1.77 (Ft 5, inch10)

TIMU ALIZOFUNDISHA

1996–2005     BASK

2006–2008     OFK Žarkovo

2008–2010     Borac

2010–2012     Resnik

2012–2013     FC Istiklol

2012–2013     Tajikistan

2014–2015     Sri Lanka

2015               New Radiant

2016               Lanexang United

2016               New Radiant

2016–2017     Saif

2017–2018     Township Rollers

2018               AFC Leopards

2018–2019     Free State Stars

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *