MASHINE HII YA KIMATAIFA YA KAZI KUFUNGA USAJILI YANGA, on August 28, 2020 at 9:00 pm

 YANGA ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Petro Atletico De Luanda ya Angola raia wa Rwanda, Jacques Tuyisenge ambaye atatambulishwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi. Kilele cha Wiki ya Mwananchi inatarajiwa kuwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi. Yanga kuelekea msimu ujao, tayari imesajili washambuliaji wanne ambao ni Michael Sarpong, Yacouba Sogne, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo ‘Carlinhos’ na Waziri Junior.Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra ni kwamba, kitendo cha kushindwa kufanya vizuri msimu uliopita, kilichangiwa zaidi na safu yao ya ushambuliaji kutokuwa imara, hivyo ndiyo sababu ya kufanya usajili bora. Mtoa taarifa huyo alisema katika kuiboresha zaidi safu yao ya ushambuliaji, wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya GSM chini ya Mkurugenzi Uwekezaji, Injinia Hersi Said wameahidi kufunga usajili na Tuyisenge. Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo utambulisho wake umeandaliwa maalum ambao utakuwa sapraizi kwa mashabiki wa timu hiyo utakaofanyika katika kilele cha Wiki ya Mwananchi. “Sapraizi kubwa imeandaliwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, kwani licha ya usajili mkubwa wa washambuliaji uliofanywa na GSM kwa kushirikiana na viongozi wa Yanga, wamepanga kufunga usajili na mshambuliaji mmoja wa kimataifa. “Mshambuliaji huyo ni Tuyisenge ambaye atatambulishwa siku hiyo, hivyo mashabiki wa Yanga wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushuhudia sapraizi hiyo. “Mashabiki wa Yanga msimu uliopita waliumia kutokana na timu yao kupata matokeo mabaya yaliyosababisha kuukosa ubingwa wa ligi kwa miaka mitatu mfululizo, hivyo katika msimu ujao hatutaki kurudia makosa,” alisema mtoa taarifa huyo. Hersi, alisikika akisema: “Bado hatujamaliza usajili wa kimataifa, wakati wowote anaweza akashuka mshambuliaji mmoja tofauti na Yacouba katika kuiimarisha safu ya ushambuliaji atakayeongozana na kocha wetu mpya Kaze.”Tayari Tuyisenge amevunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande mbili kati yake na klabu anayoichezea ya Petro Atletico De Luanda aliyojiunga nayo msimu uliopita akisaini mkataba wa miaka mitatu.,


 YANGA ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Petro Atletico De Luanda ya Angola raia wa Rwanda, Jacques Tuyisenge ambaye atatambulishwa kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

 

Kilele cha Wiki ya Mwananchi inatarajiwa kuwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo siku hiyo, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir kutoka Burundi.

 

Yanga kuelekea msimu ujao, tayari imesajili washambuliaji wanne ambao ni Michael Sarpong, Yacouba Sogne, Carlos Stenio Fernandes Guimaraes do Carmo ‘Carlinhos’ na Waziri Junior.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra ni kwamba, kitendo cha kushindwa kufanya vizuri msimu uliopita, kilichangiwa zaidi na safu yao ya ushambuliaji kutokuwa imara, hivyo ndiyo sababu ya kufanya usajili bora.

 

Mtoa taarifa huyo alisema katika kuiboresha zaidi safu yao ya ushambuliaji, wadhamini wa timu hiyo, Kampuni ya GSM chini ya Mkurugenzi Uwekezaji, Injinia Hersi Said wameahidi kufunga usajili na Tuyisenge.

 

Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo utambulisho wake umeandaliwa maalum ambao utakuwa sapraizi kwa mashabiki wa timu hiyo utakaofanyika katika kilele cha Wiki ya Mwananchi.

 

“Sapraizi kubwa imeandaliwa katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, kwani licha ya usajili mkubwa wa washambuliaji uliofanywa na GSM kwa kushirikiana na viongozi wa Yanga, wamepanga kufunga usajili na mshambuliaji mmoja wa kimataifa.

 

“Mshambuliaji huyo ni Tuyisenge ambaye atatambulishwa siku hiyo, hivyo mashabiki wa Yanga wanatakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushuhudia sapraizi hiyo.

 

“Mashabiki wa Yanga msimu uliopita waliumia kutokana na timu yao kupata matokeo mabaya yaliyosababisha kuukosa ubingwa wa ligi kwa miaka mitatu mfululizo, hivyo katika msimu ujao hatutaki kurudia makosa,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Hersi, alisikika akisema: “Bado hatujamaliza usajili wa kimataifa, wakati wowote anaweza akashuka mshambuliaji mmoja tofauti na Yacouba katika kuiimarisha safu ya ushambuliaji atakayeongozana na kocha wetu mpya Kaze.”


Tayari Tuyisenge amevunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande mbili kati yake na klabu anayoichezea ya Petro Atletico De Luanda aliyojiunga nayo msimu uliopita akisaini mkataba wa miaka mitatu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *