MESSI AINGIA ANGA ZA JUVENTUS, on August 29, 2020 at 6:46 am

IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Juventus ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi ili aungane na timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.Mabosi hao wa Juventus wanahitaji kumuunganisha Messi na mshambuliaji wao matata, Cristiano Ronaldo ili waunde pacha ya ushambuliaji bora duniani.Messi amekuwa akiripotiwa kuwa anahitaji kuondoka Barcelona ili apate changamoto mpya kwa kile anachoeleza kuwa hapendezwi na mwendo wa timu hiyo kwa sasa hasa baada ya kudhalilishwa kwa kuchapwa mabao 8-2 na Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.Kocha Mkuu wa Juventus, Andrea Pirlo anatajwa kutaka kuunganisha nguvu za washambuliaji hao ambao wana ushindani mkubwa jambo ambalo inaelezwa kuwa linaweza kuwa gumu kukamilika kwenye ulimwengu wa michezo.Mbali na Juventus Manchester City imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kupata saini ya Messi ambaye ameshawahi kufanya kazi na Pep Guardiola.,


IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Juventus ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya nyota wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi ili aungane na timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.

Mabosi hao wa Juventus wanahitaji kumuunganisha Messi na mshambuliaji wao matata, Cristiano Ronaldo ili waunde pacha ya ushambuliaji bora duniani.

Messi amekuwa akiripotiwa kuwa anahitaji kuondoka Barcelona ili apate changamoto mpya kwa kile anachoeleza kuwa hapendezwi na mwendo wa timu hiyo kwa sasa hasa baada ya kudhalilishwa kwa kuchapwa mabao 8-2 na Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha Mkuu wa Juventus, Andrea Pirlo anatajwa kutaka kuunganisha nguvu za washambuliaji hao ambao wana ushindani mkubwa jambo ambalo inaelezwa kuwa linaweza kuwa gumu kukamilika kwenye ulimwengu wa michezo.

Mbali na Juventus Manchester City imekuwa ikipewa nafasi kubwa ya kupata saini ya Messi ambaye ameshawahi kufanya kazi na Pep Guardiola.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *