Morrison awa kivutio mazoezi, on August 19, 2020 at 10:24 am

NA WINFRIDA MTOI KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ndiye aliyeiteka shoo nzima katika mazoezi ya kikosi hicho yanayoendelea kwenye uwanja wa Mo Simba Arena iliyopo Bunju, Dar es Salaam. Morrison aliyesajiliwa kwa mbwembwe uliogubikwa na utata mwingi uliosababisha kuingia katika mgogoro na uongozi wa timu yake ya zamani Yanga, ni kama anajua kuwa kila
The post Morrison awa kivutio mazoezi appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ndiye aliyeiteka shoo nzima katika mazoezi ya kikosi hicho yanayoendelea kwenye uwanja wa Mo Simba Arena iliyopo Bunju, Dar es Salaam.

Morrison aliyesajiliwa kwa mbwembwe uliogubikwa na utata mwingi uliosababisha kuingia katika mgogoro na uongozi wa timu yake ya zamani Yanga, ni kama anajua kuwa kila shabiki anamtazama yeye.

Mchezaji huyo raia wa Ghana aliyetua nchini Januari mwaka huu, amekuwa ni kipenzi kikubwa cha mashabiki wa soka kutokana na vionjo vyake vya kuchezea mpira uwanjani.

Moja ya mitindo ya Morrison iliyowateka mashabiki wa soka ni kitendo chake cha kupanda mpira akiwa uwanjani wakati mechi inaendelea.

Morrison alikuwa akizitoa Burudani hizo akiwa Yanga, lakini baada ya kuhamia Simba ameanza nazo mazoezini, hali inayowavuta mashabiki na wapenda soka wengi wanaojitokeza kushuhudia mazoezi yao.

Mchezaji huyo ameingia Msimbazi akiwa na uchangamfu wa hali ya juu, kana kwamba ni sehemu aliyokuwa akitamani kucheza kwa muda mrefu, hali iliyowafanya wadau wa timu hiyo wanaofika mazoezi kuhakikisha haondoki bila kupiga nao picha.

Ilitarajiwa kina Larry Bwalya na Chris Mugalu ndiyo watakuwa kivutio kikubwa kwa kuwa bado ni wageni nchini, lakini Morrison ameonekana ndio kipenzi cha Wanamsimbazi hao kati ya nyota wote wapya.

Mwenyewe mara kadha amesisitiza kuwa, ametimiza ndoto zake kupata nafasi ya kuichezea timu hiyo na kuahidi kuwapa raha mashabiki.

The post Morrison awa kivutio mazoezi appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *