MSHAMBULIAJI MPYA MBIKINAFASO AWASOTESHA YANGA UWANJA WA NDEGE, on August 29, 2020 at 7:07 am

 MAMIA ya mashabiki wa Yanga, Agosti 27 walijikuta wakishinda mchana kutwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kumpokea mshambuliaji wao mpya, Yacouba Sogne ambaye ilishindikana kutua nchini. Awali, Yanga kwa kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alitoa taarifa za kuwasili kwa mshambuliaji huyo saa 7:20 mchana kwa ndege aina ya Ethiopia Airline akitokea Burkina Fasso. Mshambuliaji huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo katika kuelekea msimu mpya wa 2020/2021 akitokea Asante Kotoko ya Ghana. Mashabiki hao walianza kufika kwenye uwanja huo wa ndege kuanzia saa nne asubuhi baadhi wakiwa wamevalia jezi zao zenye rangi kijani na njano zenye chapa ya Kampuni ya GSM. Kundi hilo la mashabiki walionekana kujazana kwenye mlango mkubwa wa kutokea abiria uliokuwepo uwanjani hapo huku wengine wakiwa wamekaa kwenye maegesho ya magari. Mamia hayo ya mashabiki baadhi walionekana kufika uwanjani hapo na magari yao ya kukodi aina ya Toyota Coaster huku wengine wakiwa na magari madogo ya binafsi, bodaboda. Mashabiki hao walionekana kuanza kutawanyika mara baada ya kauli ya Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz kutoa taarifa za mshambuliaji kutua leo kupitia mtandao wa Instagram. “Mshambuliaji wetu Yacouba hatakuja tena leo (jana) na badala yake atakuja kesho (leo), hivyo niwatake mashabiki wa Yanga kufuatilia taarifa mbalimbali kupitia mitandao yetu ya kijamii,” alisema Nugaz.Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo alikwama nchini Burkina Faso na anatarajiwa kuanza safari kesho ya kuja Bongo.,


 MAMIA ya mashabiki wa Yanga, Agosti 27 walijikuta wakishinda mchana kutwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kumpokea mshambuliaji wao mpya, Yacouba Sogne ambaye ilishindikana kutua nchini.

 

Awali, Yanga kwa kupitia Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli alitoa taarifa za kuwasili kwa mshambuliaji huyo saa 7:20 mchana kwa ndege aina ya Ethiopia Airline akitokea Burkina Fasso.

 

Mshambuliaji huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo katika kuelekea msimu mpya wa 2020/2021 akitokea Asante Kotoko ya Ghana.

 

Mashabiki hao walianza kufika kwenye uwanja huo wa ndege kuanzia saa nne asubuhi baadhi wakiwa wamevalia jezi zao zenye rangi kijani na njano zenye chapa ya Kampuni ya GSM.

 

Kundi hilo la mashabiki walionekana kujazana kwenye mlango mkubwa wa kutokea abiria uliokuwepo uwanjani hapo huku wengine wakiwa wamekaa kwenye maegesho ya magari.

 

Mamia hayo ya mashabiki baadhi walionekana kufika uwanjani hapo na magari yao ya kukodi aina ya Toyota Coaster huku wengine wakiwa na magari madogo ya binafsi, bodaboda.

 

Mashabiki hao walionekana kuanza kutawanyika mara baada ya kauli ya Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz kutoa taarifa za mshambuliaji kutua leo kupitia mtandao wa Instagram.

 

“Mshambuliaji wetu Yacouba hatakuja tena leo (jana) na badala yake atakuja kesho (leo), hivyo niwatake mashabiki wa Yanga kufuatilia taarifa mbalimbali kupitia mitandao yetu ya kijamii,” alisema Nugaz.


Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo alikwama nchini Burkina Faso na anatarajiwa kuanza safari kesho ya kuja Bongo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *