,, on August 28, 2020 at 11:27 am

SIMBA NI RAHA TUPU *Kwa safu hii ya ushambuliaji, watu watapigwa mabao mpaka wakimbie *Luis atua na mkewe, kikosi hichoo Arusha kuiwinda Ngao ya Jamii NA MOHAMED KASSARA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amelianzisha katika vita ya namba ya washambuliaji wake wawili, John Bocco, Chris Mugalu na Meddie Kagere ambayo mwisho wa siku, itakuwa,

SIMBA NI RAHA TUPU

*Kwa safu hii ya ushambuliaji, watu watapigwa mabao mpaka wakimbie

*Luis atua na mkewe, kikosi hichoo Arusha kuiwinda Ngao ya Jamii

NA MOHAMED KASSARA

KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amelianzisha katika vita ya namba ya washambuliaji wake wawili, John Bocco, Chris Mugalu na Meddie Kagere ambayo mwisho wa siku, itakuwa ni mtaji kwa klabu hiyo.

Kauli ya Sven ya kuanza na mshambuliaji mmoja kati ya Bocco, Mugalu na Kagere katika kikosi cha kwanza, itaibua vita nzito baina ya wapachika mabao hao kwenye kikosi hicho msimu ujao, hivyo atakayepangwa, hatataka kufanya makosa zaidi ya kupiga mabao ‘kama hana akili’.

Sven alisema anaumiza kichwa kuchagua nani aanze kati ya watatu hao katika mfumo wa 4:2:3:1 ambao anapenda kuutumia kwenye timu yake.

Baada ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya KMC na Transit Camp iliyochezwa mwanzoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Sven alisema: “Naweza kuwa na machaguo ya kumtumia mshambuliaji mmoja  kwa maana Bocco au Mugalu au wakati mwingine nikawatumia wawili, Charles  Ilanfya na Meddie Kagere kulingana na aina ya mchezo na wapinzani walivyo.

Kwanini ni vita ya Bocco, Mugalu na Kagere? Kwa sababu Sven anapenda kutumia mfumo ambao unakuwa na mshambuliaji mmoja. Lakini pia Bocco ndiye aliyekuwa akifiti kwenye mfumo huo msimu uliopita, hivyo kupata nafasi ya kucheza mbele ya Kegere.

Kagere ni aina ya mshambuliaji anayefanya vizuri katika mfumo wa 4:4:2 ambao unajumuisha washambuliaji wawili, alifanya vizuri msimu juzi chini Patrick Aussems aliyekuwa akiwaanzisha sambamba na Bocco katika mfumo wa 4:3:3.

Licha ya kuibuka kinara wa mabao katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo, lakini Kagere alipoteza nafasi chini ya Sven kutokana na kutofiti katika mfumo unaomtaka kucheza peke yake kama mshambuliaji.

Bocco alionekana kufiti katika mfumo huo kwani licha ya kufunga, alikuwa kiunganishi muhimu katika eneo la ushambuliaji  na aliinufaisha timu kutengeneza mabao mengi akisaidiana na Clatous Chama, Deo Kanda na Francis Kahata.

Hata hivyo, kwenye usajili wa dirisha hili, Simba imemwongeza Mugalu katika eneo hilo kuwapa upinzani wawili hao waliocheza kwa pamoja kwa misimu miwili mfululizo.

Kiwango alichoonesha Mugalu katika kilele cha kuadhiamisha siku ya klabu hiyo, maarufu kama Simba Day Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, kinampa wakati mgumu Sven kuamua amuanzishe nani kati ya wawili hao.

Dakika ya 45 alizocheza, zilitosha kuthibitisha ubora wake, akipambana vilivyo na mabeki wa Vital’O na mara nyingi alikuwa sahihi katika uamuzi wake.

Mugalu alianza vema kwa kufungua akaunti ya mabao kwenye kikosi cha Simba, akioneka ni mmalizaji mzuri kwani katika nafasi mbili alizopata, moja aliweka mpira kimiani.

Umbo kubwa, nguvu na matumizi mazuri ya akili, akiwa katika eneo la hatari, mabeki hawatapata nafasi ya kupumua kwani ni msumbufu kwelikweli, lakini pia akiweza kuwa kiunganishi kizuri kwenye eneo la mwisho la Simba kama alivyo Bocco.

Mcongomani huyo anajua kukaa kwenye nafasi na atakuwa moto zaidi pale atakapozoea mfumo na kuzoeana na wenzake kama Chama, Morrison na Luis Miquissone.

Ni kutokana na hali hiyo, ni wazi msimu ujao, straika yeyote atakayepewa nafasi, atahakikisha anaitendea haki kwa kutumia kila nafasi ya kufunga bao atakayoipata, hivyo kuwapa raha wapenzi wa Simba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *