Sarpong apewa mikoba ya Makambo,, on August 24, 2020 at 8:32 am

NA ZAINAB IDDY MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Michael Sarpong amekabidhiwa jezi namba 19 aliyokuwa akiitumia Heritier Makambo aliyetimkia Horoya FC ya Guinea. Sarpong amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga akitokea Rayon Sports ya Rwanda na kukabidhiwa uzi huo ambao mtangulizi wake aliutendea haki kwa kufunga mabao 16 msimu wa 2018/19. Mghana huyo atakuwa na mtihani,

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Michael Sarpong amekabidhiwa jezi namba 19 aliyokuwa akiitumia Heritier Makambo aliyetimkia Horoya FC ya Guinea.

Sarpong amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga akitokea Rayon Sports ya Rwanda na kukabidhiwa uzi huo ambao mtangulizi wake aliutendea haki kwa kufunga mabao 16 msimu wa 2018/19.

Mghana huyo atakuwa na mtihani wa kuitendea haki jezi hiyo, lakini pia kuruka kihunzi kilichowashinda Sadney Urikhob, Maybin Kalengo, Juma Balinya na David Molinga msimu uliopita.

Sarpong wachezaji wengine wapya wa timu hiyo, Tusila Kisinda na Mukoko Tonombe wote kutoka AS Vita ya DR Congo, Farid Mussa (CD Tenerife, Hispania), Zawadi Mauya (Kagera Sugar), Yassin Moustapha (Polisi Tanzania), Wazir Junior (Mbao FC) na Yacouba Songne aliyetua Jangwani kama mchezaji huru.

Wengine ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’ (huru), Kibwana Shomari (Mtibwa Sugar) na Carlos Carlinhos kutoka Interclube ya Angola.

Wachezaji hao wanatarajiwa kutambulishwa rasmi Jumamosi hii katika kilele cha Wiki ya Wananchi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Sarpong alisema anayo furaha kujiunga Yanga, huku akiahidi kuwapa raha Wanajagwani hao.
“Ninafurahi kuwa mwanafamilia wa Yanga, ninatambua kwamba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wazuri, hivyo nitakachofanya ni kutimiza majukumu yangu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,” alisema Sarpong.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *