Tuisila, Mukoko wasubiriwa kwa hamu, on August 19, 2020 at 10:26 am

NA WINFRIDA MTOI HASIRA za Wanajangwani zinaonekana kupoozwa na usajili uliofanywa hivi karibuni na uongozi wa klabu hiyo wa kuchomoa vifaa viwili katika kikosi cha kwanza cha AS Vita ya DR Congo. Wachezaji hao ambao wamekuwa gumzo muda mfupi tangu kusajiliwa Jangwani ni kiungo Mukoko Tonombe na winga Tuisila Kisinda, kila mmoja akisaini kandarasi ya
The post Tuisila, Mukoko wasubiriwa kwa hamu appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

HASIRA za Wanajangwani zinaonekana kupoozwa na usajili uliofanywa hivi karibuni na uongozi wa klabu hiyo wa kuchomoa vifaa viwili katika kikosi cha kwanza cha AS Vita ya DR Congo.

Wachezaji hao ambao wamekuwa gumzo muda mfupi tangu kusajiliwa Jangwani ni kiungo Mukoko Tonombe na winga Tuisila Kisinda, kila mmoja akisaini kandarasi ya miaka miwili.

Nyota hao walionyofolewa katika kikosi kilichowatoa jasho Simba wakati wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wamekuwa faraja kwa Wanajangwani wakiamini sasa msimu ujao watani zao hawatawasumbua.

Hamu ya kila Mwanayanga ni kuwaona wachezaji hao ‘live’ wakiwa ndani ya kikosi cha Jangwani kwa sababu usajili wao umefanyika nchini kwao na bado hawajatua katika ardhi ya Bongo.

Sababu nyingine inayowafanya mashabiki wa Yanga kuwasubiri kwa hamu Mukoko na Kisinda, ni kutokana na machungu waliyopata baada ya kuporwa Bernard Morrison.

Mashabiki hao wamepanga kufanya mapokezi makubwa ya wachezaji hao, endapo wataruhusiwa na uongozi wa timu hiyo kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said ambaye alipanda ndege kwenda DR Congo kukamilisha usajili huo, kuanzia kesho vifaa hivyo vinaanza kuwasili nchini.

“Mukoko na Kisinda tayari ni wachezaji wa Yanga, kuanzia Alhamisi wanaweza kuwasili Tanzania kujiunga na timu mazoezini, pia wapo wachezaji wengine, mshambulaji wetu Yacouba Songne na mwingine tutakayemsajili,” alisema.

The post Tuisila, Mukoko wasubiriwa kwa hamu appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *