WAJUMBE WALILAZA ZEGE LA MORRISON, on August 12, 2020 at 1:53 pm

NA WINFRIDA MTOI NGOMA bado ngumu katika sakata la winga Mghana, Bernard Morrison, baada ya wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kutoa uamuzi. Sakata hilo lilianza kusikilizwa juzi kuanzia asubuhi hadi usiku na kushindwa kufikia muafaka licha ya pande zote kuwepo katika kikao, huku ikiahidiwa kukamilika
The post WAJUMBE WALILAZA ZEGE LA MORRISON appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

NGOMA bado ngumu katika sakata la winga Mghana, Bernard Morrison, baada ya wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kushindwa kutoa uamuzi.

Sakata hilo lilianza kusikilizwa juzi kuanzia asubuhi hadi usiku na kushindwa kufikia muafaka licha ya pande zote kuwepo katika kikao, huku ikiahidiwa kukamilika jana lakini imeshindikana tena.

Morrison ameingia katika mgogoro na klabu yake ya Yanga ikipinga kitendo cha kusaini mkataba na klabu hiyo na kisha kuonekana picha zinazomuonyesha akisaini kwa watani wao Simba, hivyo suala hilo kupelekwa TFF.

Kabla uamuzi haujatolewa, Morrison akatambulishwa na Simba kupitia mtandao wao akionekana anasaini mkataba miaka miwili kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu ujao.

Kitendo hicho kililifanya sakata hilo kuendelea kuwa gumzo na kuwafanya mashabiki kujazana katika ofisi za Makao Makuu ya TFF Ilala jijini Dar es Salaam, kusubiri hatma ya nyota huyo, lakini mambo yamekuwa magumu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji TFF, Elias Mwanjala, alisema sababu ya kushindwa kutolewa uamuzi jana kama walivyoahidi ni kutokana na kutokamilika nyaraka kwa pande zote mbili.

Alisema wamekubaliana kila kitu kipatikane leo na kikao hicho kitaanza saa 4:00 asubuhi ambapo pia uamuzi utatolewa.

The post WAJUMBE WALILAZA ZEGE LA MORRISON appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *