Wazawa Yanga wapewa vidonge vyao,, on August 27, 2020 at 8:13 am

NA ZAINAB IDDY ASILIMIA 80 ya uongozi wa juu wa Yanga, uliweka kambi ya saa nne kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam, wakati wa mazoezi ya timu hiyo jana, kujiandaa na msimu ujao. Yanga imeanza maandalizi hayo wiki tatu zilizopita chini ya kocha wa viungo, Riedoh Berdien kabla ya Juma Mwambusi kuitwa,

NA ZAINAB IDDY

ASILIMIA 80 ya uongozi wa juu wa Yanga, uliweka kambi ya saa nne kwenye Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar es Salaam, wakati wa mazoezi ya timu hiyo jana, kujiandaa na msimu ujao.

Yanga imeanza maandalizi hayo wiki tatu zilizopita chini ya kocha wa viungo, Riedoh Berdien kabla ya Juma Mwambusi kuitwa akiwa kama kocha msaidizi.

Katika kipindi chote hicho cha mazoezi, kwa mara ya kwanza, uongozi wa juu wa Yanga, umetua mazoezini jana na kushuhudia wachezaji wao wanachokifanya.

Katika mazoezi hayo ya jana, viongozi waliotinga mazoezini ni Mwenyekiti Mshindo Msolla, Makamu wake, Fedrick Mwakalebela, Senzo Mbatha (Mshauri), Mkurugezi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said  pamoja na wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji.

Kabla ya kuanza mazoezi yao, Dk. Msolla alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji, ikiwamo kumtambulisha Mwambusi kwa viongozi wengine pamoja na wachezaji.

Mara baada ya utambulisho huo, Msolla aliwataka wachezaji kufanya kazi kwa ushirikiano kwa maslahi ya Yanga pamoja na wao binafsi.

“Mafanikio ambayo timu itayapata kupitia kazi mtakayoifanya wachezaji, hayataenda Yanga tu, bali hata mchezaji mmoja mmoja atakuwa mejitengenezea nafasi nzuri ya kujitangaza kimataifa,” alisema.

Kwa upande wake, Hersi alisema: “Msimu wa 2020/21 hatutaki mchezo katika timu, yale masikhara na uzembe uliokuwa unafanyika kipindi kilichopita, yameishia kule, tunahitaji matokeo ya ushindi tu na si vingine.

“Lazima mtambue tumetumia gharama kubwa kuijenga upya timu na bado tunafanya mengi kwa faida ya Yanga ambayo kama itafanikiwa, bila shaka hata wachezaji itawagusa, kwa sababu hakutakuwa na tatizo la mishahara, lakini pia posho zitatolewa nyingi… hii ina mana kazi nzuri mtakayoifanya, ndiyo itazaa matunda katika timu.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *