Posted By Posted On

COASTAL UNION KUTAMBULISHA MAJEMBE 19, on August 30, 2020 at 10:01 am

UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa hauna presha na suala la usajili kwa sasa kwa kuwa umejipanga vema kwa kuwasajili wachezaji wapya 19 ikiwa ni idadi ya wachezaji ambao wameondoka.Kwa sasa Coastal Union imeuza  wachezaji saba wa kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto aliyekwenda Simba, Ibrahim Ame yupo Yanga, Ayoub Lyanga,Azam FC,Muhsin Malima, Serbia,Andrew Simba,Azam FC,Makiada Franko, Mbao FC na Sudi Dondola KMC huku ikiwaacha jumla wachezaji 12.Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Coastal Union, JJuma Mgunda alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na mashaka kwa kuwa utaratibu wa usajili wameshamaliza kilichobaki ni kuwatambulisha wachezaji.“Tupo kimya lakini mambo yanakwenda, dirisha la usajili linafungwa tarehe 31, sasa tuhangaike na nini katika kuwatangaza wachezaji wetu? Hatuna presha na mashabiki niwatoe mashaka kwamba tumeshasajili sawa na idadi ya wachezaji ambao wameondoka na tutawatambulisha kabla ya dirisha kufungwa,” alisema Mgunda. ,


UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa hauna presha na suala la usajili kwa sasa kwa kuwa umejipanga vema kwa kuwasajili wachezaji wapya 19 ikiwa ni idadi ya wachezaji ambao wameondoka.

Kwa sasa Coastal Union imeuza  wachezaji saba wa kikosi cha kwanza ambao ni Bakari Mwamnyeto aliyekwenda Simba, Ibrahim Ame yupo Yanga, Ayoub Lyanga,Azam FC,Muhsin Malima, Serbia,Andrew Simba,Azam FC,Makiada Franko, Mbao FC na Sudi Dondola KMC huku ikiwaacha jumla wachezaji 12.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Coastal Union, JJuma Mgunda alisema kuwa mashabiki wa timu hiyo wasiwe na mashaka kwa kuwa utaratibu wa usajili wameshamaliza kilichobaki ni kuwatambulisha wachezaji.

“Tupo kimya lakini mambo yanakwenda, dirisha la usajili linafungwa tarehe 31, sasa tuhangaike na nini katika kuwatangaza wachezaji wetu? Hatuna presha na mashabiki niwatoe mashaka kwamba tumeshasajili sawa na idadi ya wachezaji ambao wameondoka na tutawatambulisha kabla ya dirisha kufungwa,” alisema Mgunda.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *