Posted By Posted On

ISHU YA YANGA KUITAKA SAINI YA CHAMA IPO HIVI, on August 30, 2020 at 8:00 am

 MJUMBE wa Kamati ya Usajili wa Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema hawakuwa na mpango kabisa wa kumsajili kiungo mchezeshaji mpya Simba raia wa Zambia, Larry Bwalya huku akisisitiza yeye alimuulizia Clatous Chama kwa meneja wake. Hivi karibuni kuliibuka tetesi za Yanga kuwepo kwenye mipango ya kumsajili Bwalya kabla ya siku chache Simba kuchukua maamuzi ya haraka kufanikisha saini ya nyota huyo.Kiungo huyo amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga hapo akitokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika huko. Akizungumza jijini Dar jana, Hersi alisema kuwa meneja wa Chama ndiye anayemsimamia Bwalya ambaye yeye alifanya mawasiliano naye kumuuliza kama kuna uwezekano wa kumpata Chama. “Meneja wa Chama ndiye huyo wa Bwalya, mimi nilichofanya kumuulizia Chama nikionyesha nia ya kumsajili, lakini sasa kilichotokea ni meneja huyo kuwapigia simu viongozi wa Simba kwa ajili ya kuwajaza. “Meneja huyo aliwapigia simu Simba kwa kuwaambia kuwa, Yanga wameonyesha nia ya kumsajili Bwalya kwa lengo la kuwaongezea kasi viongozi hao ili kukamilisha dili hilo la usajili haraka. “Huyo Bwalya hatukuwa katika mipango naye kabisa, Chama kweli lakini siyo huyo kiungo, nikuhakikishie kuwa Yanga tukihitaji jambo letu hivi hakuna wa kulizuia kama tulivyoamua kwa Mwamnyeto (Bakari) kumsajili. “Tunafahamu moja ya klabu kubwa ambayo pinzani (Simba) ilikuwa ikitangaza kuwa Mwamnyeto ndiye mchezaji wao, lakini mwisho wa siku amekuja Yanga,” amesema.,

 


MJUMBE wa Kamati ya Usajili wa Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, amesema hawakuwa na mpango kabisa wa kumsajili kiungo mchezeshaji mpya Simba raia wa Zambia, Larry Bwalya huku akisisitiza yeye alimuulizia Clatous Chama kwa meneja wake.

 

Hivi karibuni kuliibuka tetesi za Yanga kuwepo kwenye mipango ya kumsajili Bwalya kabla ya siku chache Simba kuchukua maamuzi ya haraka kufanikisha saini ya nyota huyo.


Kiungo huyo amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili kukipiga hapo akitokea Power Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika huko.

 

Akizungumza jijini Dar jana, Hersi alisema kuwa meneja wa Chama ndiye anayemsimamia Bwalya ambaye yeye alifanya mawasiliano naye kumuuliza kama kuna uwezekano wa kumpata Chama.

 

“Meneja wa Chama ndiye huyo wa Bwalya, mimi nilichofanya kumuulizia Chama nikionyesha nia ya kumsajili, lakini sasa kilichotokea ni meneja huyo kuwapigia simu viongozi wa Simba kwa ajili ya kuwajaza.

 

“Meneja huyo aliwapigia simu Simba kwa kuwaambia kuwa, Yanga wameonyesha nia ya kumsajili Bwalya kwa lengo la kuwaongezea kasi viongozi hao ili kukamilisha dili hilo la usajili haraka.

 

“Huyo Bwalya hatukuwa katika mipango naye kabisa, Chama kweli lakini siyo huyo kiungo, nikuhakikishie kuwa Yanga tukihitaji jambo letu hivi hakuna wa kulizuia kama tulivyoamua kwa Mwamnyeto (Bakari) kumsajili.

 

“Tunafahamu moja ya klabu kubwa ambayo pinzani (Simba) ilikuwa ikitangaza kuwa Mwamnyeto ndiye mchezaji wao, lakini mwisho wa siku amekuja Yanga,” amesema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *