Posted By Posted On

JEMBE LA YANGA JIPYA KUTUA LEO, on August 30, 2020 at 9:00 pm

 MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga,Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso anatarajiwa kutua nchini leo Agosti 31, akitokea nchini Burkina Faso. Nyota huyo ilibidi atue nchini Agosti 27 na mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JINA) ila alishindwa kutua na alikosa tamasha la Wananchi lililofanyika jana Uwanja wa Mkapa ambapo wachezaji wapya na jezi mpya ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ilitambulishwa.  Yacouba alimalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kuisha na anakuja akiwa ni mchezaji huru. Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema kuwa ndege yake ilizuiliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 30. Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo baada ya kutua nchini,  ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi na tayari wachezaji wa Yanga walianza mazoezi Agosti 10.  “Agosti 31 atawasili nchini na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi,” alisema Injinia.  ,

 MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga,Yacouba Sogne raia wa Burkina Faso anatarajiwa kutua nchini leo Agosti 31, akitokea nchini Burkina Faso.

 

Nyota huyo ilibidi atue nchini Agosti 27 na mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JINA) ila alishindwa kutua na alikosa tamasha la Wananchi lililofanyika jana Uwanja wa Mkapa ambapo wachezaji wapya na jezi mpya ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 ilitambulishwa.

 

 Yacouba alimalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kuisha na anakuja akiwa ni mchezaji huru.

 

Kwa mujibu wa Mjumbe wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema kuwa ndege yake ilizuiliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 30.

 

Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo baada ya kutua nchini,  ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi na tayari wachezaji wa Yanga walianza mazoezi Agosti 10.

  

“Agosti 31 atawasili nchini na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi,” alisema Injinia.

 

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *