Posted By Posted On

SAKATA LA MORRISON LAIBUKA UPYA, YANGA WAMTAMBULISHA UWANJA WA MKAPA, on August 30, 2020 at 3:33 pm

 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison ni mali yao na wamemtambulisha kuwa mchezaji wao wa 28.Leo Agosti 30, Uwanja wa Mkapa ni siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo wanatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2019/20 na timu hiyo.Wakati wa utambulisho wa wachezaji hao ambao wametambulishwa na Mtangazaji na Mwadishi wa Wasafi Media ambae pia ni mchambuzi ndani ya Gazeti la Championi, Maulid Kitenge amesema kuwa bado Morrison ni mchezaji wa Yanga.Katika utambulisho huo Kitenge amesema:”Mchezaji wa 28 ndani ya Yanga ni Bernard Morrison ambaye ni mchezaji wetu kwa kuwa kesi ipo CAS hivyo ni mchezaji wa Yanga.”Sakata la Morrison lilidumu ndani ya Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa muda wa siku tatu na baadaye maamuzi yalitolewa kuwa Morrison ni mchezaji huru hivyo anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote anayohitaji.Agosti 8, alisaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba na amecheza mechi siku ya Kilele cha Simba day Agosti 22 wakati Simba ikicheza na Vital’O ya Burundi na ilishinda mabao 6-0 huku yeye akifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.Leo pia Agosti 30 amecheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. ,

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado mchezaji wao wa zamani Bernard Morrison ni mali yao na wamemtambulisha kuwa mchezaji wao wa 28.

Leo Agosti 30, Uwanja wa Mkapa ni siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi ambapo wanatambulisha wachezaji wapya na wale waliokuwa na kikosi hicho kwa msimu wa 2019/20 na timu hiyo.


Wakati wa utambulisho wa wachezaji hao ambao wametambulishwa na Mtangazaji na Mwadishi wa Wasafi Media ambae pia ni mchambuzi ndani ya Gazeti la Championi, Maulid Kitenge amesema kuwa bado Morrison ni mchezaji wa Yanga.


Katika utambulisho huo Kitenge amesema:”Mchezaji wa 28 ndani ya Yanga ni Bernard Morrison ambaye ni mchezaji wetu kwa kuwa kesi ipo CAS hivyo ni mchezaji wa Yanga.”


Sakata la Morrison lilidumu ndani ya Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa muda wa siku tatu na baadaye maamuzi yalitolewa kuwa Morrison ni mchezaji huru hivyo anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote anayohitaji.


Agosti 8, alisaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba na amecheza mechi siku ya Kilele cha Simba day Agosti 22 wakati Simba ikicheza na Vital’O ya Burundi na ilishinda mabao 6-0 huku yeye akifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.


Leo pia Agosti 30 amecheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC wakati Simba ikishinda mabao 2-0, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid. 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *