Posted By Posted On

SIKU MPYA YA JEMBE JIPYA YA YANGA KUTUA HII HAPA, on August 30, 2020 at 5:00 am

 MJUMBE wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia mshambuliaji wao kipenzi raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne atatua nchini Agosti 31, mwaka huu. Agosti 27 mashabiki wa timu hiyo walijitokeza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINA) jijini Dar kumpokea mshambuliaji huyo ambaye baadaye ilishindikana kuwasili. Yacouba ni kati ya washambuliaji wa timu hiyo waliosajiliwa akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na timu hiyo, kama mchezaji huru. Kwa mujibu wa Hersi, ndege yake ilizuliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 31, mwaka huu kabla ya siku inayofuatia kutua nchini. Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo mara baada ya kutua nchini, haraka ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi. “ Hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya mashabiki na uongozi, kwani ndege aliyotakiwa kuja nayo Yacouba ilizuiliwa kutua nchini kutokana na sababu zao. “Hivyo atajiunga na timu Agosti 31 na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa” alisema Hersi. ,

 


MJUMBE wa Kamati ya Usajili Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia mshambuliaji wao kipenzi raia wa Burkina Faso, Yacouba Sogne atatua nchini Agosti 31, mwaka huu.

 

Agosti 27 mashabiki wa timu hiyo walijitokeza kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINA) jijini Dar kumpokea mshambuliaji huyo ambaye baadaye ilishindikana kuwasili.

 

Yacouba ni kati ya washambuliaji wa timu hiyo waliosajiliwa akitokea Asante Kotoko ya Ghana mara baada ya mkataba wake kumalizika na kujiunga na timu hiyo, kama mchezaji huru.

 

Kwa mujibu wa Hersi, ndege yake ilizuliwa kutua nchini hivyo amekatiwa tiketi nyingine na atatoka kwao Burkina Faso Agosti 31, mwaka huu kabla ya siku inayofuatia kutua nchini.

 

Hersi alisema kuwa mshambuliaji huyo mara baada ya kutua nchini, haraka ataungana na kambi ya pamoja kwa ajili ya kuanza mazoezi ya pamoja kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

 

“ Hakukuwa na mawasiliano mazuri kati ya mashabiki na uongozi, kwani ndege aliyotakiwa kuja nayo Yacouba ilizuiliwa kutua nchini kutokana na sababu zao.

 

“Hivyo atajiunga na timu Agosti 31 na hatakuwepo kwenye kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa” alisema Hersi.

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *