Posted By Posted On

AFC YAFUNGWA MABAO 6-0 NA SIMBA, LUIS MIQUSSONE ATUPIA MATATU, on August 31, 2020 at 5:12 pm

 KIKOSI cha Simba, leo Agosti 31 kimeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya AFC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya nne kwa pasi ya Ibrahim Ajibu ndani ya 18, bao la pili lilifungwa na Larry Bwalya dakika ya 24 kwa pasi ya Ajibu na bao la tatu lilifungwa na Kagere dakika ya 34 kwa pasi ya Gadiel Michael. Mpaka muda wa mapumziko Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 huku AFC ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45.Kipindi cha pili Simba ilipachika mabao mengine matatu kupitia kwa kiungo wao Luis Miqussone aliyefunga ‘hat trick’ ambapo alifunga bao la nne dakika ya 64  kwa shuti la nje ya 18 baada ya kipa wa AFC kutema mpira.Bao la tano lilipachikwa dakika ya 76 kwa pasi ya Said Ndemla na kuzamisha bao kambani na bao la sita lilipachikwa dakika ya 88 baada ya mabeki wa AFC kujichanganya namna ya kukaba.Simba wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na AFC wao wanajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.,

 

KIKOSI cha Simba, leo Agosti 31 kimeibuka na ushindi wa mabao 6-0 mbele ya AFC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. 


Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya nne kwa pasi ya Ibrahim Ajibu ndani ya 18, bao la pili lilifungwa na Larry Bwalya dakika ya 24 kwa pasi ya Ajibu na bao la tatu lilifungwa na Kagere dakika ya 34 kwa pasi ya Gadiel Michael. 


Mpaka muda wa mapumziko Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 huku AFC ikiwa haijaambulia bao ndani ya dakika 45.


Kipindi cha pili Simba ilipachika mabao mengine matatu kupitia kwa kiungo wao Luis Miqussone aliyefunga ‘hat trick’ ambapo alifunga bao la nne dakika ya 64  kwa shuti la nje ya 18 baada ya kipa wa AFC kutema mpira.


Bao la tano lilipachikwa dakika ya 76 kwa pasi ya Said Ndemla na kuzamisha bao kambani na bao la sita lilipachikwa dakika ya 88 baada ya mabeki wa AFC kujichanganya namna ya kukaba.


Simba wanajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6 Uwanja wa Sokoine na AFC wao wanajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *