Posted By Posted On

HAMAD HILIKA ASAJILIWA MTIBWA SUGAR NA KUFUNGA MABAO MAWILI KATIKA USHINDI WA 6-2 LEO GAIRO, on August 31, 2020 at 4:08 pm

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAMKLABU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ kutoka Zimamoto ya Zanzibar.Hilika anacheza nafasi ya ushambuliaji, mfungaji bora mara mbili ligi kuu Zanzibar msimu 2019/2020 na 2016/2017, Pia amewahi kuibuka mfungaji bora katika kombe la Mapinduzi Cup.Hilika almaarufu striker wa nchi amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha wana tam tam.Mtibwa Sugar imemsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad ‘Hilika’ kutoka Zimamoto ya Zanzibar Hilika pia ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Zanzibar Heroes, Huu ni usajili wetu wa nane na mwisho kuelekea msimu wa 2020/2021.Wengine wapya Mtibwa Sugar ni Abubakar Ame Omar AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan.Wakati huo huo: Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 6-2 dhidi Kombaini ya Gairo katika mchezo kirafiki Uwanja wa CCM Gairo. Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Boban Zirintusa, Ibrahim Hilika mawili kila mmoja na Abdul Haule moja.,

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KLABU ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kumsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad Ahmada ‘Hilika’ kutoka Zimamoto ya Zanzibar.
Hilika anacheza nafasi ya ushambuliaji, mfungaji bora mara mbili ligi kuu Zanzibar msimu 2019/2020 na 2016/2017, Pia amewahi kuibuka mfungaji bora katika kombe la Mapinduzi Cup.
Hilika almaarufu striker wa nchi amesaini mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi cha wana tam tam.

Mtibwa Sugar imemsajili mshambuliaji Ibrahim Hamad ‘Hilika’ kutoka Zimamoto ya Zanzibar 

Hilika pia ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Zanzibar Heroes, Huu ni usajili wetu wa nane na mwisho kuelekea msimu wa 2020/2021.
Wengine wapya Mtibwa Sugar ni Abubakar Ame Omar AbalKassim Khamis, Baraka Gamba Majogoro, George Makanga, Geofrey Luseke na Hassan Kessy Ramadhan.
Wakati huo huo: Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 6-2 dhidi Kombaini ya Gairo katika mchezo kirafiki Uwanja wa CCM Gairo. 
Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Boban Zirintusa, Ibrahim Hilika mawili kila mmoja na Abdul Haule moja.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *