Posted By Posted On

MANE ANUKIA BARCELONA, on August 31, 2020 at 11:00 am

 SADIO Mane nyota wa Klabu ya Liverpool anatajwa kuingia anga za Klabu ya Barcelona ili kuziba pengo la mshambuliaji wao namba moja Lionel Messi ambaye anatajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho.Mane raia wa Senegal  amekuwa chachu kubwa ya mafanikio ndani ya Liverpool ambayo msimu wa 2019/20 ilitwaa taji la Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 30 pia alikuwa kwenye kikosi kilichotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.Amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah pamoja na nyota mwingine Roberto Firmino wakiunda utatu wao matata ndani ya kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Anfield kwa mechi za nyumbani.Ripoti zinaeleza kuwa Mane anataka kwenda Barcelona ili akafanye kazi na kocha mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walifanya naye kazi alipokuwa akikinoa kikosi cha Southampton.Alipofanya kazi na kocha huyo Mane alifunga mabao 25 kwenye jumla ya mechi 75 alizocheza anaamini kwamaba akitua hapo atapata nafasi ya kurejesha makali yake zaidi.,


 SADIO Mane nyota wa Klabu ya Liverpool anatajwa kuingia anga za Klabu ya Barcelona ili kuziba pengo la mshambuliaji wao namba moja Lionel Messi ambaye anatajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Mane raia wa Senegal  amekuwa chachu kubwa ya mafanikio ndani ya Liverpool ambayo msimu wa 2019/20 ilitwaa taji la Ligi Kuu England baada ya kupita miaka 30 pia alikuwa kwenye kikosi kilichotwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na nyota wa Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah pamoja na nyota mwingine Roberto Firmino wakiunda utatu wao matata ndani ya kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Anfield kwa mechi za nyumbani.

Ripoti zinaeleza kuwa Mane anataka kwenda Barcelona ili akafanye kazi na kocha mpya wa klabu hiyo Ronald Koeman ambaye kwa sasa yupo ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walifanya naye kazi alipokuwa akikinoa kikosi cha Southampton.

Alipofanya kazi na kocha huyo Mane alifunga mabao 25 kwenye jumla ya mechi 75 alizocheza anaamini kwamaba akitua hapo atapata nafasi ya kurejesha makali yake zaidi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *