Posted By Posted On

MCHEZO MZIMA WA SIMBA KUTWAA NGAO YA JAMII ULIKUWA NAMNA HII, on August 31, 2020 at 8:39 am

 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck jana Agosti 30 kilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kushinda mchezo wa fainali mbele ya Namungo FC kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.Timu zote mbili dakika tano za mwanzo zilianza kwa kasi na dakika ya nne, nahodha wa Simba John Bocco alikosa nafasi ya wazi kwa pasi kutoka kwa Hassan Dilunga ndani ya 18 na Clatous Chama naye alipiga shuti liliokolewa na mlinda mlango wa Namungo, Nurdin Barola.IIliwachukua dakika mbili Simba kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya saba na Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya kiungo mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18 na mchezaji wa Namungo, Steven Duah aliyeonyeshwa kadi ya njano dakika ya saba.Penalti hiyo iliwafanya wachezaji wa Namungo kumfuata mwamuzi wakionekana kumlalamikia ila hakubadili maamuzi yake.Baada ya Simba kupata bao waliacha kushambulia na kuanza kucheza kwa pasi nyingi kipindi cha kwanza mpaka dakika 45 kukamilika kwa Simba wakiwa mbele kwa bao 1-0.Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika twakwimu zilionyesha kuwa Simba ilipiga jumla ya mashuti manne huku Namungo wakipiga shuti moja  langoni,na kwa upande wa faulo Namungo na Simba wote walicheza jumla ya faulo 12.Umiliki wa mpira kwa Simba ilikuwa asilimia 62 na Namungo 38.Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na walipata bao la pili kupitia kwa Morrison dakika ya 60 akimalizia pasi ya Clatous Chama.Kwenye mchezo huo kiungo mkabaji, Jonas Mkude alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa fainali na alipewa kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni zawadi yake.Simba ilikabidhiwa Ngao ya Jamii na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo , Harrison Mwakyembe pia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia naye alikuwepo pia.Kikosi cha SimbaAishi Manula, Shomari Kapombe/Kameta, Mohamed Hussein,Joash Onyango,Kenned Juma,Jonas Mkude,Hassan Dilunga,Muzamiru Yassin,John Bocco/Kagere,Clatous Chama/Ajib na Bernard Morrison/Bwalya. Kikosi cha Namungo FCNourdine Barola,Rogers Gabriel/Shamte,Jaffary Mohamed,Steven Duah,Hamis Fakhi/Kyaka,Humoud Abdulharim/Khalifa,Abeid Athuman/Blaise,Lucas Kikoti,Steven Sey,Nzigamasabo Styve na Sixtus Sabilo/Shiza Kichuya ,

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck jana Agosti 30 kilifanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kwa kushinda mchezo wa fainali mbele ya Namungo FC kwa ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Timu zote mbili dakika tano za mwanzo zilianza kwa kasi na dakika ya nne, nahodha wa Simba John Bocco alikosa nafasi ya wazi kwa pasi kutoka kwa Hassan Dilunga ndani ya 18 na Clatous Chama naye alipiga shuti liliokolewa na mlinda mlango wa Namungo, Nurdin Barola.

IIliwachukua dakika mbili Simba kupata bao la kuongoza lililofungwa dakika ya saba na Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya kiungo mshambuliaji wa Simba Bernard Morrison kuchezewa faulo ndani ya 18 na mchezaji wa Namungo, Steven Duah aliyeonyeshwa kadi ya njano dakika ya saba.

Penalti hiyo iliwafanya wachezaji wa Namungo kumfuata mwamuzi wakionekana kumlalamikia ila hakubadili maamuzi yake.

Baada ya Simba kupata bao waliacha kushambulia na kuanza kucheza kwa pasi nyingi kipindi cha kwanza mpaka dakika 45 kukamilika kwa Simba wakiwa mbele kwa bao 1-0.

Mpaka dakika 45 za mwanzo zinakamilika twakwimu zilionyesha kuwa Simba ilipiga jumla ya mashuti manne huku Namungo wakipiga shuti moja  langoni,na kwa upande wa faulo Namungo na Simba wote walicheza jumla ya faulo 12.Umiliki wa mpira kwa Simba ilikuwa asilimia 62 na Namungo 38.

Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na walipata bao la pili kupitia kwa Morrison dakika ya 60 akimalizia pasi ya Clatous Chama.

Kwenye mchezo huo kiungo mkabaji, Jonas Mkude alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa fainali na alipewa kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni zawadi yake.


Simba ilikabidhiwa Ngao ya Jamii na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo , Harrison Mwakyembe pia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia naye alikuwepo pia.

Kikosi cha Simba

Aishi Manula, Shomari Kapombe/Kameta, Mohamed Hussein,Joash Onyango,Kenned Juma,Jonas Mkude,Hassan Dilunga,Muzamiru Yassin,John Bocco/Kagere,Clatous Chama/Ajib na Bernard Morrison/Bwalya.

 

Kikosi cha Namungo FC

Nourdine Barola,Rogers Gabriel/Shamte,Jaffary Mohamed,Steven Duah,Hamis Fakhi/Kyaka,Humoud Abdulharim/Khalifa,Abeid Athuman/Blaise,Lucas Kikoti,Steven Sey,Nzigamasabo Styve na Sixtus Sabilo/Shiza Kichuya

 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *