Posted By Posted On

Simba yaweka rekodi nyingine,, on August 31, 2020 at 8:37 am

NA MWANDISHI WETU ACHANA na rekodi za Simba ambazo ziliwekwa hivi karibuni kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo kama ilivyokuwa kwa watani zao Yanga. Pia, kushinda mataji hao kwa tofauti ya pointi nyingi. Kubwa zaidi, wakali hao wa mitaa ya Msimbazi kuweka Ngao ya Jamii ya sita katika kabati lao,

NA MWANDISHI WETU

ACHANA na rekodi za Simba ambazo ziliwekwa hivi karibuni kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo kama ilivyokuwa kwa watani zao Yanga. Pia, kushinda mataji hao kwa tofauti ya pointi nyingi.

Kubwa zaidi, wakali hao wa mitaa ya Msimbazi kuweka Ngao ya Jamii ya sita katika kabati lao na kuwa timu iliyoshinda mara nyingi zaidi ya klabu yoyote tangu ilipoanza mwaka 2001, kisha kurejea miaka nane baadae.

Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, ulitosha kwa Simba kuwapiku Yanga ambao wanayo matano kwenye kabati lao pale Jangwani.

Pia, Simba inakuwa timu ya kwanza kushinda Ngao ya Jamii mara nne mfululizo, ingawa, awali hakukuwa na timu iliyowahi kufanya hivyo mara tatu. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara walishinda mwaka 2017, 2018, 2019 na 2020.

Timu zingine zilizowahi kushinda Ngao ya Jamii ni Azam na Mtibwa Sugar, ambazo kila moja imefanya hivyo mara moja katika historia.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *