Posted By Posted On

Sven atoa onyo Simba,, on September 1, 2020 at 6:52 am

NA WINFRIDA MTOI WAKATI wapenzi wa Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelea kutamba msimu ujao, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, amewaonya vikali, akiwaambia haitakuwa rahisi kihivyo kama wanavyofikiria. Msimu uliopita, ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Simba, wakifanikiwa kutwaa mataji matatu, wakianzia na Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa,

NA WINFRIDA MTOI

WAKATI wapenzi wa Simba wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelea kutamba msimu ujao, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, amewaonya vikali, akiwaambia haitakuwa rahisi kihivyo kama wanavyofikiria.

Msimu uliopita, ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Simba, wakifanikiwa kutwaa mataji matatu, wakianzia na Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa tatu mfululizo na lile la Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).

Kutokana na kile wanachoamini kuwa na kikosi imara na kipana, watu wa Simba wamekuwa wakitamba kuendeleza moto wao msimu ujao.

Tayari Wekundu wa Msimbazi hao wameufungua msimu mpya wa 2020/21 kwa kishindo kwa kutwaa Ngao ya Jamii juzi walipoichapa Namungo FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Lakini kwa Sven, yeye yupo tofauti na mashabiki, wanachama na baadhi ya viongozi wa Simba, akisema msimu wa 2020/2021 utakuwa mgumu kwao kuliko uliopita kutokana na usajili uliofanywa na timu mpinzani.

Akizungumza na mtandao wa klabu yao juzi, Sven alisema msimu uliopita walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakiwa na michezo sita mkononi, kitu ambacho hatarajii kukiona kikitatokea msimu huu wa 2020/21 kutokana na ubora timu nyingine.

“Msimu wa 2020/2021utakuwa mgumu kwa sababu timu zimesajili wachezaji wazuri, msimu uliopita tuliweka historia ya kutwaa ubingwa ikiwa bado michezo sita, sitarajii kutokea hivyo,” alisema.

Alisema ili waweze kutamba msimu huu, watatakiwa kufanya kazi ya ziada, kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, viongozi ha hata mashabiki wao.

“Iwapo tutaingia msimu mpya tukiwa na imani kuwa sisi ni bora kuliko wengine, tutakuwa tunajidanganya na mwisho wa siku, tunaweza kujikuta tukishindwa kufikia malengo yetu,” alisema.

Aliwataka wapenzi wa Simba, wachezaji na viongozi kushikamana na kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ili kufikia malengo yao waliyojiwekea ya kuendelea kutamba msimu huu mpya.

Juu ya kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake juzi dhidi ya Namungo, Sven alisema wamemridhisha, ukizingatia wamefanya mazoezi kwa wiki mbili tu.

Alisema nyota wake waliweza kumiliki mpira kwa alisilimia 90 na kufanya mashabulizi ya hatari kwa Namungo, hivyo muda uliobaki watautumia kuzidi kujiimarisha zaidi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *