Posted By Posted On

FIRST 11 YANGA IMETIMIA, on September 2, 2020 at 9:51 am

NA WINFRIDA MTOI KIU ya Wanayanga ya muda mrefu ya kuwa na kikosi cha kwanza kilichosheni wachezaji wenye viwango, imemalizika baada ya kuona usajili mzuri uliofanywa msimu huu. Aliyekamilisha usajili wa kikosi hicho ni straika, Yacouba Sogne, aliyewasili juzi na kufunga pazia la usajili klabuni hapo. Baada ya kusuasua msimu uliopita, Yanga imeamua kufanya kweli
The post FIRST 11 YANGA IMETIMIA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI
KIU ya Wanayanga ya muda mrefu ya kuwa na kikosi cha kwanza kilichosheni wachezaji wenye viwango, imemalizika baada ya kuona usajili mzuri uliofanywa msimu huu.
Aliyekamilisha usajili wa kikosi hicho ni straika, Yacouba Sogne, aliyewasili juzi na kufunga pazia la usajili klabuni hapo.
Baada ya kusuasua msimu uliopita, Yanga imeamua kufanya kweli kwa kushusha vifaa vya nguvu kabla ya dirisha la usajili kufungwa jana, ambavyo vinatarajia kurejesha heshima Jangwani.
Ikumbukwe kuwa kikosi cha Yanga msimu uliopita kilikuwa na upungufu katika baadhi ya maeneo kwa kukosa wachezaji wenye uwezo wa kuleta ushindani na hivyo kuambulia nafasi ya pili.
Hali hiyo ilisababisha mabingwa hao wa kihistoria kushindwa kuchukua taji lolote na kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Kutokana na usajili huo, pamoja na kuboresha benchi la ufundi, Yanga sasa ina jeuri ya kutambia kikosi chake chenye ‘First 11’ imara pamoja na wachezaji wa akiba wenye viwango.
Kulingana na wachezaji waliosajiliwa, ‘first 11’ ya msimu huu itakuwa na nyota kama Farouk Shikalo, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Tonombe Mukoko, Farid Mussa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Michael Sarpong, Yacoub Songne na Tuisila Kisinda.
Pamoja na kikosi hicho, ukingalia katika benchi nako si haba kwani utakutana na kina Haruna Niyonzima, Carlos Carlinhos na wengine ambao wamesajiliwa kipindi hiki na wale wa msimu uliopita.
Wachezaji kama Carlinhos na Yacouba hawajapata muda wa kuonesha vitu vyao mbele ya Wanajangwani hao, licha ya Carlinhos kucheza dakika 10 siku ya kilele cha Wiki ya Wananchi lakini hajamaliza kiu ya wapenzi wa timu hiyo.
Yacouba yeye alitua nchini juzi, hivyo hajaonekana hata akigusa mpira akiwa ndani ya kikosi cha timu hiyo, ni dhahiri kila Mwanayanga ana hamu ya kuona vitu vyake ndani ya dakika 90.
Ndani ya siku nne zilizobaki, benchi la ufundi la Yanga, lina kazi ya ziada kuhakikisha linatengeneza kikosi cha kwanza kitakachowapa matokeo mazuri katika mechi za awali.
Kwa kulifahamu hilo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi, aliweka wazi kuwa wana wachezaji wengi wenye vipaji katika kikosi hicho na wataangalia jinsi ya kukipanga katika kipindi hiki kifupi kabla ya kuanza ligi Jumapili ijayo.
“Tutatumia muda uliopo kupata kikosi imara huku tukiendelea kutengeneza muunganiko kwa sababu wachezaji wengi ni wageni,” alisema.
Mwambusi alifafanua kuwa kinachowapa matumaini ni kwamba wachezaji wote waliosajiliwa wana viwango vizuri na uzoefu wa kutumia vipaji vyao.
Timu hiyo itafungua pazia la Ligi Kuu Bara kwa kuikaribisha Tanzania Prisons Septemba 6, katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

The post FIRST 11 YANGA IMETIMIA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *