Posted By Posted On

KIBWANA, MUSTAFA ULINZI KAMILI YANGA, on September 2, 2020 at 10:30 am

NA WINFRIDA MTOI KATIKA suala la ulinzi wa pembeni, Yanga imeshamaliza kazi kutokana na majembe mawili waliyoyasajili, Kibwana Shomari, mlinzi wa kulia na Yassin Mustafa upande wa kushoto kuwa katika kiwango kizuri. Wachezaji hao wamedhihirisha kuwa Yanga, haijafanya makosa kutokana na kiwango walichokionesha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir kwenye Uwanja wa Mkapa,
The post KIBWANA, MUSTAFA ULINZI KAMILI YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

KATIKA suala la ulinzi wa pembeni, Yanga imeshamaliza kazi kutokana na majembe mawili waliyoyasajili, Kibwana Shomari, mlinzi wa kulia na Yassin Mustafa upande wa kushoto kuwa katika kiwango kizuri.

Wachezaji hao wamedhihirisha kuwa Yanga, haijafanya makosa kutokana na kiwango walichokionesha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Aigle Noir kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Shomari aliyesajiliwa na Yanga kutoka Mtibwa Sugar, amekuwa akihakikisha anaziba pengo la Juma Abdul aliyeachwa akisaidiana na Paul Godfrey ‘Boxer’.

Kwa upande wa Mustafa yeye ameonesha wazi kuwa yuko fiti kwa kuondoa tatizo la muda mrefu la beki wa kushoto ambalo baadhi ya wachezaji waliosajiliwa msimu uliopita walishindwa.

Hata hivyo benchi la ufundi ndilo litakuwa na jukumu la kuchagua ni mchezaji gani anaweza kuendana na mfumo na kasi ya Wanajangwani hao wanaopigania kurudisha heshima ya kwa kutwaa ubingwa msimu ujao.

The post KIBWANA, MUSTAFA ULINZI KAMILI YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *