Posted By Posted On

SVEN VANDENBROEC AFUNGUKIA ISHU YAKE NA KAGERE, on September 2, 2020 at 11:16 am

 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hana tatizo na nyota namba moja wa kucheza na nyavu ndani ya Simba Meddie Kagere.Habari zinaeleza kuwa wawili hao walipigana jana baada ya kutofautiana jambo ambalo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku uongozi wa Simba ukikanusha kwamba hakuna ukweli katika hilo.Sven amesema kuwa:- “Siwezi kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi. Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema.”Kagere ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo amesepa na tuzo ya mfungaji bora ambapo msimu wa 2018/19 ikiwa ni msimu wake wa kwanza alitupia mabao 23.Msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22 na kufanya afikishe jumla ya mabao 45 ndani ya Ligi Kuu Bara.Kwa sasa Simba imeanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine, Mbeya dhidi ya Ihefu.,

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hana tatizo na nyota namba moja wa kucheza na nyavu ndani ya Simba Meddie Kagere.


Habari zinaeleza kuwa wawili hao walipigana jana baada ya kutofautiana jambo ambalo lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku uongozi wa Simba ukikanusha kwamba hakuna ukweli katika hilo.

Sven amesema kuwa:- “Siwezi kutumia nguvu kwenye mambo yasiyo ya maana ambayo sijui yanatoka wapi. Mimi sina tatizo, Medie hana tatizo hilo ndilo ninaweza kusema.”

Kagere ndani ya Bongo kwa misimu miwili mfululizo amesepa na tuzo ya mfungaji bora ambapo msimu wa 2018/19 ikiwa ni msimu wake wa kwanza alitupia mabao 23.

Msimu wa 2019/20 alitupia mabao 22 na kufanya afikishe jumla ya mabao 45 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa Simba imeanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine, Mbeya dhidi ya Ihefu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *