Posted By Posted On

UMEISIKIA SIKU YA MORRISON NA LUIS?, on September 2, 2020 at 12:26 pm

NA WINFRIDA MTOI UMEWASIKIA Simba? Baada ya kunogewa na vitu vya Bernard Morrison, hamu yao kubwa ni kumuona mchezaji huyo akiwa anacheza kikosi kimoja na Luis Miquissone. Morrison aliyesajiliwa na Wanamsimbazi hao, tayari ameshatupia mabao mawili katika michezo miwili aliyocheza tangu amesajiliwa mwezi uliopita akitokea Yanga. Kiungo huyo mshambuliaji, alifunga bao la kwanza akiwa Msimbazi,
The post UMEISIKIA SIKU YA MORRISON NA LUIS? appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

UMEWASIKIA Simba? Baada ya kunogewa na vitu vya Bernard Morrison, hamu yao kubwa ni kumuona mchezaji huyo akiwa anacheza kikosi kimoja na Luis Miquissone.

Morrison aliyesajiliwa na Wanamsimbazi hao, tayari ameshatupia mabao mawili katika michezo miwili aliyocheza tangu amesajiliwa mwezi uliopita akitokea Yanga.

Kiungo huyo mshambuliaji, alifunga bao la kwanza akiwa Msimbazi, wakati wa mechi ya   Simba Day dhidi ya Vital’O ya Burundi katika ushindi wa mabao 6-0 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Nyota huyo aliendelea kuwakosha Wanamsimbazi baada ya kutupia bao lingine katika mechi ya Ngao ya Jamii, wakati Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC, Uwanja Sheik Amri Abeid jijini Arusha.

Katika mechi zote hizo, Morrison alionesha kiwango cha hali ya juu, hivyo mashabiki wa Simba wanatamani kumuona akiwa na Luis ambaye hakucheza mechi zote mbili.

Wanachohitaji Wanasimba ni kumuona Luis akiwa anacheza winga ya kulia huku Morrison akikichafua winga ya kushoto, wakiamini itakuwa ni burudani nzuri kutokana na kasi na mbwembwe za wachezaji wote wawili.

Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, juzi alieleza kufurahishwa na kiwango alichoonyesha Luis akiifungia timu yake mabao matatu katika matokeo ya ushindi wa mabao 6-0 walioupata dhidi ya Arusha FC.

The post UMEISIKIA SIKU YA MORRISON NA LUIS? appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *