Posted By Posted On

Bodi ya Ligi yawapiga mkwara mzito waamuzi,, on September 3, 2020 at 8:16 am

NA ZAINAB IDDY BODI ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), imesema msimu ujao wa 2020/21 hawatawafumbia macho waamuzi ambao watashindwa kutafsiri sheria 17 za soka kwa maslahi binafsi. Akizungumza na BINGWA jana, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, alisema msimu uliopita ulikuwa na malalamiko mengi kwa waamuzi.  “Yapo  malalamiko ambayo yalifanyiwa kazi na Kamati,

NA ZAINAB IDDY

BODI ya Ligi Tanzania Bara (TPLB), imesema msimu ujao wa 2020/21 hawatawafumbia macho waamuzi ambao watashindwa kutafsiri sheria 17 za soka kwa maslahi binafsi.

Akizungumza na BINGWA jana, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo, alisema msimu uliopita ulikuwa na malalamiko mengi kwa waamuzi.

 “Yapo  malalamiko ambayo yalifanyiwa kazi na Kamati ya Waamuzi baada ya kufika mezani, lakini mengi yalishindwa kuchukuliwa hatua kwa sababu hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

“Bodi ambayo ina dhamana ya Ligi za Tanzania, msimu huu tutafuatilia kila mechi itakayochezwa kuanzia Daraja la Pili (SDL), Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Kuu  (VPL) na ikitokea tukabaini kuna mapungufu kwa yeyote hatutasita kuingilia kati ili kuhakikisha hatua stahiki inachukuliwa na wale watakaobainika kufanya mchezo mchafu.”

Kasongo aliongeza: “Tunahitaji ligi ya msimu huu iwe ya tofauti kubwa na zile zilizotangulia hasa katika kuhakikisha waamuzi wanatimiza wajibu wao kikamilifu kwa sababu tunaamini wao ndio chanzo cha kuharibu mchezo  mzima pale watakapofanya maamuzi kinyume na sheria 17 zilizowekwa,”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *