Posted By Posted On

IHEFU YAPANIA KUIONESHA SIMBA,, on September 3, 2020 at 8:11 am

NA VICTORIA GODFREY UONGOZI wa Klabu ya Ihefu, umesema kikosi chao kinajipanga kuonesha ubora wao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sokeine, jijini Mbeya. Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka mkoani Mbeya, Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew, alisema wachezaji wao  wanaendelea kujiandaa kuhakikisha wanapata,

NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Klabu ya Ihefu, umesema kikosi chao kinajipanga kuonesha ubora wao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Sokeine, jijini Mbeya.

Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka mkoani Mbeya, Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew, alisema wachezaji wao  wanaendelea kujiandaa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya Simba.

Andrew alisema licha ya kwamba hawajawahi kukutana na Simba katika mchezo wowote, lakini amaini wachezaji wao watapambana na baadaye kushinda.

“Tumejiaandaa  vizuri  japo wao ni klabu kubwa kuliko sisi, lakini dakika 90 zitakupa mwamba  nini. Tupo tayari  kushindana na lazima tushindane.

“Yanga na Azam  hawa  tulicheza  nao katika michuano ya FA, hivyo lazima tuoneshe ubora wetu mbele ya Simba na tupate alama,”alisema  Andrew.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *