Posted By Posted On

KAGERE AFUNGUKIA ISHU YAKE KUDAIWA KUMPIGA SVEN, on September 3, 2020 at 1:19 pm

MEDDIE Kagere, mshambuliaji namba moja wa Klabu ya Simba amesema amesikitishwa na taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa amempiga kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck. Septemba Mosi taarifa za Kagere kudaiwa kumpiga kocha huyo kisa kikiwa ni kutopangwa kikosi cha kwanza cha Simba zilizagaa kwa kasi mitandaoni, na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.  Mshambuliaji huyo amesema ameshangaa baada ya kuona mambo hayo yanasambaa wakati yeye hajafanya tukio hilo. “Kuna mambo huwa yanasemwa kuhusu mimi ambayo siyo ya kweli yenye lengo la kunichafua ndiyo maana sijawahi kuwajibu.“Lilianza la hirizi nikanyamaza na sasa limekuja la mimi kupigana na kocha kitu ambacho siyo kweli. nashangaa sijui mwalimu nimempiga wapi,” amesema Kegere.Uongozi wa Simba SC kupitia Ofisa Habari Haji Manara umekanusha taarifa hizo kwa kusema hazina ukweli, zaidi ya kutaka kuvuruga amani ndani ya kikosi chao ambacho kipo tayari kuanza kutetea taji la Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili dhidi ya Ihefu FC. Haji Manara amesema: ”Wanasema ugomvi uliotokea mazoezini, lakini Simba hawakuwa na mazoezi baada ya mchezo wa ngao ya jamii, hizo ni propaganda za kuvuruga utulivu uliopo ndani na nje ya Simba, wakitaka itokee kama upande wa pili yanayoendelea. “Kama idara ya Habari na Mawasiliano hatutokubali kuona watu wanaandika uzushi kuhusu klabu yetu na tutachukua hatua kali dhidi ya watakaohusika.”,


MEDDIE Kagere, mshambuliaji namba moja wa Klabu ya Simba amesema amesikitishwa na taarifa zilizosambaa mtandaoni kuwa amempiga kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck.

 

Septemba Mosi taarifa za Kagere kudaiwa kumpiga kocha huyo kisa kikiwa ni kutopangwa kikosi cha kwanza cha Simba zilizagaa kwa kasi mitandaoni, na kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

 

 Mshambuliaji huyo amesema ameshangaa baada ya kuona mambo hayo yanasambaa wakati yeye hajafanya tukio hilo.

 

“Kuna mambo huwa yanasemwa kuhusu mimi ambayo siyo ya kweli yenye lengo la kunichafua ndiyo maana sijawahi kuwajibu.


“Lilianza la hirizi nikanyamaza na sasa limekuja la mimi kupigana na kocha kitu ambacho siyo kweli. nashangaa sijui mwalimu nimempiga wapi,” amesema Kegere.


Uongozi wa Simba SC kupitia Ofisa Habari Haji Manara umekanusha taarifa hizo kwa kusema hazina ukweli, zaidi ya kutaka kuvuruga amani ndani ya kikosi chao ambacho kipo tayari kuanza kutetea taji la Tanzania Bara mwishoni mwa juma hili dhidi ya Ihefu FC.

 

Haji Manara amesema: ”Wanasema ugomvi uliotokea mazoezini, lakini Simba hawakuwa na mazoezi baada ya mchezo wa ngao ya jamii, hizo ni propaganda za kuvuruga utulivu uliopo ndani na nje ya Simba, wakitaka itokee kama upande wa pili yanayoendelea.

 

“Kama idara ya Habari na Mawasiliano hatutokubali kuona watu wanaandika uzushi kuhusu klabu yetu na tutachukua hatua kali dhidi ya watakaohusika.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *