Posted By Posted On

MBWANA SAMATTA ACHEKELEA KUBAKI EPL, on September 2, 2020 at 5:13 pm

 NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ataendelea kukipiga katika Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England. Aston Villa imenusurika kushuka daraja msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35. Timu hiyo ilifanikiwa kubaki baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham inayofundishwa na kocha David Moyes. Samatta amesema:-. “Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine tena, napenda kuwashukuru mashabiki waliokuwa nyuma yangu, kuiombea Villa kubaki msimu ujao, nawaomba waendelee kuomba ili na mimi niendelee kubaki hapa,” alisema Samatta. Samatta alijiunga na Klabu ya Aston Villa akitokea Genk ya Ubelgiji kwa kitita cha pauni milioni 8.5 (zaidi ya sh bil. 25 za Tanzania).Kwa sasa tayari Aston Villa imeanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu England inayotarajiwa kuanza Septemba 12.,

 


NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ataendelea kukipiga katika Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England.

 

Aston Villa imenusurika kushuka daraja msimu huu, baada ya kumaliza nafasi ya 17 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 35. Timu hiyo ilifanikiwa kubaki baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na West Ham inayofundishwa na kocha David Moyes.

 

Samatta amesema:-. Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine tena, napenda kuwashukuru mashabiki waliokuwa nyuma yangu, kuiombea Villa kubaki msimu ujao, nawaomba waendelee kuomba ili na mimi niendelee kubaki hapa,” alisema Samatta.

 

Samatta alijiunga na Klabu ya Aston Villa akitokea Genk ya Ubelgiji kwa kitita cha pauni milioni 8.5 (zaidi ya sh bil. 25 za Tanzania).


Kwa sasa tayari Aston Villa imeanza maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu England inayotarajiwa kuanza Septemba 12.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *