Posted By Posted On

Meja Mingange atua Lipuli FC,, on September 3, 2020 at 10:11 am

NA ZAINAB IDDY ALIYEKUWA wa  timu ya Ndanda, Meja Mstaafu wa Jeshi  Abdull Mingange, amejiunga na kikosi cha Lipuli  kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara. Meja Mingange ambaye amewahi  kuzifundisha timu za Mbeya City na Azam msimu uliopita alikuwa na Ndanda  iliyoshuka daraja. Akizungumza   na BINGWA jana, Meja,

NA ZAINAB IDDY

ALIYEKUWA wa  timu ya Ndanda, Meja Mstaafu wa Jeshi  Abdull Mingange, amejiunga na kikosi cha Lipuli  kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.

Meja Mingange ambaye amewahi  kuzifundisha timu za Mbeya City na Azam msimu uliopita alikuwa na Ndanda  iliyoshuka daraja.

Akizungumza   na BINGWA jana, Meja Mingange alisema baada ya kumalizana na Ndanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha Lipuli.

Meja Mingange alisema baada ya Ndanda kushuka daraja viongozi wa klabu hiyo  hawakutaka aendelee kuifundisha na sasa amejiunga na Lipulil.

“Hapa Lipuli nimekuja kwa kazi maalumu ya kuisadia kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022 na hilo kwangu sio kazi kwa sababu naanza nayo msimu mpya.

 “Nimeshiriki katika usajili wa wachezaji wapya ambao bila shaka watakuwa chachu ya ushindani ndani ya kikosi na  katika mashindano ili mwisho kwa pamoja tuweze kutimiza lengo,” alisema Meja Mingange.

Lipuli ilimaliza nafasi ya 18  kutokana na pointi 44, baada ya kucheza michezo  38 msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *