Posted By Posted On

Ngasa, Tegete waipa matumaini Ndanda,, on September 3, 2020 at 8:19 am

NA ZAINAB IDDY BAADA ya  wachezaji wawili Mrisho Ngasa na Jeryson Tegete,  kutua  Ndanda, Uongozi wa klabu hiyo umesema nyota hawa watairejesha timu yao Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2021. Ngasa na Tegete waliowahi kucheza pamoja wakiwa Yanga na Taifa Stars, wamejiunga na Ndanda inayojiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ,baada ya kushuka daraja,

NA ZAINAB IDDY

BAADA ya  wachezaji wawili Mrisho Ngasa na Jeryson Tegete,  kutua  Ndanda, Uongozi wa klabu hiyo umesema nyota hawa watairejesha timu yao Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2021.

Ngasa na Tegete waliowahi kucheza pamoja wakiwa Yanga na Taifa Stars, wamejiunga na Ndanda inayojiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza ,baada ya kushuka daraja msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Katibu Mkuu wa Klabu ya Ndanda, Seleman Kachele, alisema pamoja na wana wachezaji wengi wazuri, lakini uwapo wa Ngassa na Tegete ni jambo lingine kutokana na uzoefu walionao katika michuano mbalimbali ya ndani na kimataifa.

“Ngassa na Tegete wameshacheza timu mbalimbali na kukutana na changamoto nyingi sana, ujio wao unafaida kubwa kwa Ndanda katika harakati za kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Kupitia Ngassa na Tegete wachezaji wengine watajifunza mambo ya msingi ambayo yataturejesha katika ligi kama watayafanyia kazi kikamilifu,” alisema Kachele.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *