Posted By Posted On

VAN de BEEK AMALIZANA NA MANCHESTER UNITED, AKABIDHIWA JEZI NAMBA 34, on September 3, 2020 at 3:00 pm

 KLABU ya Manchester United ya England imekamilisha usajili wa mchezaji Donny van de Beek (23) kwa ada ya Paundi Milioni 40 kutokea Klabu ya Ajax ya Uholanzi.Van de Beek amesaini kandarasi ya miaka mitano kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi na inaelezwa kuwa atalipwa Paundi 107,000 kwa wiki pamoja na marupurupu.Huu ni usajili wa kwanza wa Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa dirisha hili la usajili ambapo Van de Beek ambaye amepewa jezi namba 34 anatarajiwa kutengeneza muunganiko mzuri katika nafasi ya kiungo pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.Solskjaer inaelezwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kusajili walau Beki mmoja wa kati na kiungo mshambuliaji wa upande wa kulia huku Jadon Sancho akiwa ndio chaguo namba moja katika eneo hilo la kiungo mshambuliaji.,


 KLABU ya Manchester United ya England imekamilisha usajili wa mchezaji Donny van de Beek (23) kwa ada ya Paundi Milioni 40 kutokea Klabu ya Ajax ya Uholanzi.

Van de Beek amesaini kandarasi ya miaka mitano kukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi na inaelezwa kuwa atalipwa Paundi 107,000 kwa wiki pamoja na marupurupu.


Huu ni usajili wa kwanza wa Kocha Ole Gunnar Solskjaer kwa dirisha hili la usajili ambapo Van de Beek ambaye amepewa jezi namba 34 anatarajiwa kutengeneza muunganiko mzuri katika nafasi ya kiungo pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.


Solskjaer inaelezwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kusajili walau Beki mmoja wa kati na kiungo mshambuliaji wa upande wa kulia huku Jadon Sancho akiwa ndio chaguo namba moja katika eneo hilo la kiungo mshambuliaji.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *