Posted By Posted On

Waamuzi watende haki msimu mpya wa 2020/21,, on September 3, 2020 at 9:15 am

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza Jumapili huku timu zikiwa katika maandalizi ya mwisho kuhakikisha zinafanya vizuri. Katika michezo ya ufunguzi itakayochezwa Jumapili, Namungo itavaana na Coastal, wakati Biashara United watakuwa nyumbani kucheza na Gwambina. Dodoma Jiji watawakaribisha Mwadui na Ihefu watacheza na Simba, Mtibwa Sugar wakivaana na Ruvu Shooting wakati Yanga wakitarajiwa kucheza na,

LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuanza Jumapili huku timu zikiwa katika maandalizi ya mwisho kuhakikisha zinafanya vizuri.

Katika michezo ya ufunguzi itakayochezwa Jumapili, Namungo itavaana na Coastal, wakati Biashara United watakuwa nyumbani kucheza na Gwambina.

Dodoma Jiji watawakaribisha Mwadui na Ihefu watacheza na Simba, Mtibwa Sugar wakivaana na Ruvu Shooting wakati Yanga wakitarajiwa kucheza na Tanzania Prisons.

Lakini timu zikiwa katika maandalizi ya msimu mpaya, Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), imesema haitamfumbia macho mwamuzi ambaye ataonekana ksuhindwa kutafsiri sheria 17 za soka.

Msimu uliopita ulimalizika kukiwa na malalamiko mengi kwa waamuzi kwa wao kushindwa kumudu vyema michezo mbalimbali na kufikia wengine kufungiwa.

Tulishuhudia baadhi ya waamuzi wakipewa onyo kali na wengine kuondolewa katika orodha ya kuchezesha ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutokana na kushindwa kufuata sheria hizo za soka.

BINGWA tunasema kwa kuwa waamuzi ndio wenye maamuzi ya mwisho tunaona msimu unaokuja wawe makini kutenda haki ili kuondoa changamoto ya msimu uliopita

Uzoefu unaonyesha baadahi ya waamuzi wanatoa uamuzi wenye utata kutokana na mapenzi yao kwa timu au kwa kushindwa kufahamu vyema sheria za soka.

Hivyo basi, huu ni muda mwafaka wa kuwaandaa waamuzi kwa maana ya kuwapa semina ili nao waweze kuzielewa kwa ufasaha sheria zinazotawala mchezo huo, tukiamini kutasaidia kuondoa changamoto.

Tunaamini kwa kufanya hivyo kutawasaidia hata wale waamuzi ambao walikuwa hawana uelewa mpana kuzielewa sheria hizo za soka.

Ni vema msimu ujao waamuzi wakachezesha kwa kufuata sheria zote 17 za soka kuhakikisha mshindi anapatikana uwanjani kulingana na kiwango chake na si fedha zake.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *