Posted By Posted On

AZAM FC WAPANIA MAKUBWA 2020/21, on September 4, 2020 at 7:00 am

 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa utakuja tofauti ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kufanya makubwa tofauti na msimu uliopita wa 2019/20 ambao ulikuwa mbovu kwao.Msimu uliopita Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ilikwama kutwaa taji lolote ikiwa ni pamoja na lile la Mapinduzi Cup, Kombe la Shirikisho, Kombe la Kagame pamoja na Ligi Kuu Bara jambo ambalo limewapa somo matajiri hao wa Dar es Salaam.Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa kwa msimu wa 2020/21 watafanya mengi makubwa kwa ajili ya mashabiki na wadau wa Azam FC kwa kuwa wamedhamiria kuleta mapinduzi.”Tupo vizuri na tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21, msimu uliopita malengo yetu yote yalikwama ila kwa sasa tunaanza upya na tunaamini tutafanya vizuri.”Ukianza na usajili tumefanya kazi kubwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu katika ushindani hivyo hatuna mashaka, mashabiki watupe sapoti,tunahitaji ubingwa,” amesema. Azam FC itamenyana na Polisi Tanzania Septemba 7, Uwanja wa Azam Complex ambapo ina wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na Prince Dube, Awesu Awesu na David Kissu.,

 

UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa utakuja tofauti ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kufanya makubwa tofauti na msimu uliopita wa 2019/20 ambao ulikuwa mbovu kwao.


Msimu uliopita Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba ilikwama kutwaa taji lolote ikiwa ni pamoja na lile la Mapinduzi Cup, Kombe la Shirikisho, Kombe la Kagame pamoja na Ligi Kuu Bara jambo ambalo limewapa somo matajiri hao wa Dar es Salaam.


Ofisa Habari wa Azam FC,  Zakaria Thabit amesema kuwa kwa msimu wa 2020/21 watafanya mengi makubwa kwa ajili ya mashabiki na wadau wa Azam FC kwa kuwa wamedhamiria kuleta mapinduzi.


“Tupo vizuri na tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21, msimu uliopita malengo yetu yote yalikwama ila kwa sasa tunaanza upya na tunaamini tutafanya vizuri.


“Ukianza na usajili tumefanya kazi kubwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu katika ushindani hivyo hatuna mashaka, mashabiki watupe sapoti,tunahitaji ubingwa,” amesema. 


Azam FC itamenyana na Polisi Tanzania Septemba 7, Uwanja wa Azam Complex ambapo ina wachezaji wapya ikiwa ni pamoja na Prince Dube, Awesu Awesu na David Kissu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *