Posted By Posted On

Azam wapiga mkwara mzito,, on September 4, 2020 at 10:54 am

NA ZAINAB IDDY KOCHA Msaidizi wa timu ya Azam FC,  Bahati Vivier, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha msimu huu wa 2020/21, wanatwaa mataji. Azam inatarajia kutupa karata yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara Jumatatu kwa kuvaana na Polisi Tanzania kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex. Akizungumza na BINGWA jana, Vivier alisema kushindwa kupata,

NA ZAINAB IDDY

KOCHA Msaidizi wa timu ya Azam FC,  Bahati Vivier, amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha msimu huu wa 2020/21, wanatwaa mataji.

Azam inatarajia kutupa karata yake ya kwanza ya Ligi Kuu Bara Jumatatu kwa kuvaana na Polisi Tanzania kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex.

Akizungumza na BINGWA jana, Vivier alisema kushindwa kupata taji lolote na kukosa nafasi ya kushiriki kimataifa  msimu uliopita, kuliwaumiza mno kama benchi la ufundi.

“Benchi la ufundi tuliumia kuona tunamaliza mashindano ya Tanzania Bara bila ya kuwa na taji, tumekaa na kutafakari kisha tukajua kitu gani tunapaswa kufanya.

“Kwanza tulihitaji usajili ambao ungetupa matokeo na uongozi umetimiza hilo, jukumu tulilonalo ni kuhakikisha timu inacheza kwa umoja na kupata matokeo na hilo tunalianza katika mechi yetu ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania,” alisema.

Katika msimu wa ulioisha wa Ligi Kuu Bara, Azam FC ilimaliza ikiwa nafasi ya tatu baada ya kukusanya pointi 70 walizozipata ndani ya michezo 38 waliyocheza, wakati katika mashindano ya FA, iliondolewa hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *