Posted By Posted On

Carlinhos aanza kufundishwa lugha,, on September 4, 2020 at 11:19 am

NA ZAINAB IDDY KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos,  amekabidhiwa kwa mchezaji wa zamani timu hiyo, Said Maulid “SMG“, ili kumsaidia mambo mbalimbali baada ya kushindwa  kuzungumza Lugha ya Kiingereza kama ilivyo kwa wenzake. Carlinhos ambaye ni raia wa Angola amesajiliwa na Yanga katika dirisha kubwa msimu huu, hivyo kukutana na changamoto ya lugha.,

NA ZAINAB IDDY

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Carlos Carlinhos,  amekabidhiwa kwa mchezaji wa zamani timu hiyo, Said Maulid SMG“, ili kumsaidia mambo mbalimbali baada ya kushindwa  kuzungumza Lugha ya Kiingereza kama ilivyo kwa wenzake.

Carlinhos ambaye ni raia wa Angola amesajiliwa na Yanga katika dirisha kubwa msimu huu, hivyo kukutana na changamoto ya lugha.

BINGWA lilimtafuta SMG  ambaye  alikiri kuwa ni  kweli  amepewa jukumu hilo  na uongozi wa Yanga huku akitoa muda wa mwezi mmoja  na Carlinhos ataanza kuwasiliana na wenzake bila ya kuhitaji msaada wa mwingine.

“Angola wana lugha yao maalumu ya kuwasiliana tofauti na Kiingereza japo kuwa wapo wanaojua Kiingereza pia, hili ni jambo la kawaida kwa wachezaji wanaotoka nchi moja kwenda nyingine   hata mimi nilipokwenda kucheza  Angola changamoto ya lugha nilikutana nayo.

“Nitamsaidia katika kuhakikisha anajua maneno muhimu ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza baada ya mwezi mmoja au miwili ataweza kuwasiliana na wenzake bila ya kuhitaji msaada wa mtu mwingine.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *