Posted By Posted On

Jeshi la Azam kamili vitani,, on September 4, 2020 at 11:08 am

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kikosi chao kimekamilika baada ya nyota wao wa kigeni kupata vibali vya kufanyia kazi nchini. Azam imetoa kauli hiyo ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza kutimua vumbi, ikitarajia kukutana na Polisi Tanzania Jumatatu ijayo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es,

NA WINFRIDA MTOI

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kikosi chao kimekamilika baada ya nyota wao wa kigeni kupata vibali vya kufanyia kazi nchini.

Azam imetoa kauli hiyo ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza kutimua vumbi, ikitarajia kukutana na Polisi Tanzania Jumatatu ijayo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, alisema wamekamilisha kila kitu kuhusu vibali vya wachezaji na mambo mengine ya kuwafanya wawe huru kuwatumia nyota wao.

Zaka alisema suala la vibali ni jambo wanalolipa kipaumbele mara, baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji wa kigeni ili kuepuka usumbufu dakika za mwisho.

“Katika mambo ambayo tunawekea msisitizo ni kufuata taratibu zote zilizowekwa na mamlaka husika za soka na serikali kwa hiyo vibali vya wachezaji wetu vimekamilika na wapo tayari kuitumikia timu,”alisema.

Kuhusu maandalizi alisema kocha anaendelea na program zake  na mechi chache  za kirafiki walizocheza zimetosha.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *