Posted By Posted On

Lamine, Mapinduzi kuikosa Prisons,, on September 4, 2020 at 11:27 am

NA ZAINAB IDDY NYOTA wa kikosi cha Yanga, Lamine Moro na Mapinduzi Balama, hawataonekana katika mechi za mwanzo za Ligi Kuu Tanzania kutokana na majeraha. Mapinduzi  aliumia mguu wa kulia wakati wakijiandaa na mechi ya  dhidi ya Ndanda FC msimu uliopita na Moro  alipata majeraha ya kifundo cha mguu  katika mazoezi ya kujiandaa na msimu,

NA ZAINAB IDDY

NYOTA wa kikosi cha Yanga, Lamine Moro na Mapinduzi Balama, hawataonekana katika mechi za mwanzo za Ligi Kuu Tanzania kutokana na majeraha.

Mapinduzi  aliumia mguu wa kulia wakati wakijiandaa na mechi ya  dhidi ya Ndanda FC msimu uliopita na Moro  alipata majeraha ya kifundo cha mguu  katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.

Akizungumza na BINGWA, Moro alisema alitamani kuanza na wenzake, lakini imekuwa ngumu kwa sababu bado hajapona  vizuri.

“Kwa sababu za kiafya sina budi kukaa nje, daktari ameniambia kuwa, nitarejea hivi karibuni lakini nasubiri vipimo zaidi ambavyo natarajia kupimwa wiki ijayo,”alisema Moro.

Balama alisema:“ Naendelea vizuri hivi sasa na nina matumaini ya kurejea uwanjani  kuanzia mwezi ujao nimekuwa nikifanyiwa ukaguzi kila baada ya wiki moja kujua maendeleo yangu.”

Panzia la Ligi Kuu msimu wa 202/21 litafunguliwa Jumapili kwa  Yanga kushuka dimbani kuumana na Tanzania Prisons kwenye la Mkapa, Dar es Salaam.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *