Posted By Posted On

MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA ANAWAZA KUFUNGA TU, on September 4, 2020 at 9:00 pm

NYOTA mpya wa Yanga, Michael Sarpong amesema kuwa ndoto yake kubwa kwa sasa ndani ya timu hiyo ni kuendelea kufunga kwa kuwa ndiyo jukumu lake kubwa. Sarpong amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sport ya Rwanda tayari ameanza kuwasha moto ndani ya kikosi cha timu hiyo kufuatia kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.Mchezo huo ulichezwa Agosti 30 kwenye kilele cha Siku ya Mwananchi jijini Dar es Salaam.  Sarpong amesema kuwa bao hilo kwake limemfungulia njia ya kuendelea kufunga zaidi katika ligi kuu inayotarajia kuanza Jumapili kwa Yanga kucheza na Prisons.“Binafsi nashukuru Mungu kwa sababu ilikuwa ndoto yangu kuona nafunga kwenye mchezo ule kwa kuwa ulikuwa muhimu kwa mashabiki ambao walikuja uwanjani kutusapoti, maana walikuwa wamejaa kwa sababu yetu. “Lakini naamini litaniongezea chachu kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika ligi, kwa sababu nipo hapa kwa kazi ya kufunga mabao, maana ndiyo jukumu langu, sasa sitaki kuona nakwama kwenye hilo, kwani nataka kufunga mabao mengi zaidi, japo ni suala gumu kwa sasa kuweka mipango yangu wazi zaidi ya kuwa msaada kwenye timu,” alisema.,


NYOTA mpya wa Yanga, Michael Sarpong amesema kuwa ndoto yake kubwa kwa sasa ndani ya timu hiyo ni kuendelea kufunga kwa kuwa ndiyo jukumu lake kubwa.

 

Sarpong amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rayon Sport ya Rwanda tayari ameanza kuwasha moto ndani ya kikosi cha timu hiyo kufuatia kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Aigle Noir ya Burundi.


Mchezo huo ulichezwa Agosti 30 kwenye kilele cha Siku ya Mwananchi jijini Dar es Salaam.

 

 Sarpong amesema kuwa bao hilo kwake limemfungulia njia ya kuendelea kufunga zaidi katika ligi kuu inayotarajia kuanza Jumapili kwa Yanga kucheza na Prisons.


“Binafsi nashukuru Mungu kwa sababu ilikuwa ndoto yangu kuona nafunga kwenye mchezo ule kwa kuwa ulikuwa muhimu kwa mashabiki ambao walikuja uwanjani kutusapoti, maana walikuwa wamejaa kwa sababu yetu.

 

“Lakini naamini litaniongezea chachu kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika ligi, kwa sababu nipo hapa kwa kazi ya kufunga mabao, maana ndiyo jukumu langu, sasa sitaki kuona nakwama kwenye hilo, kwani nataka kufunga mabao mengi zaidi, japo ni suala gumu kwa sasa kuweka mipango yangu wazi zaidi ya kuwa msaada kwenye timu,” alisema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *