Posted By Posted On

MUGALU NYOTA MPYA WA SIMBA KUIKOSA IHEFU MAZIMA, on September 4, 2020 at 9:46 am

 MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, tayari yupo nchini  baada ya kurudi kutoka nyumbani kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia ila ataukosa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine.Mugalu ni kati ya wachezaji wapya wa kimataifa waliosajiliwa na Simba katika kukiimarisha kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck. Wengine ni Larry Bwalya, Bernard Morrison na Joash Onyango.Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Lusaka Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kumalizika.Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven, amesema kuwa mshambuliaji huyo tayari ametua nchini baada ya kumaliza ruhusa ya wiki moja aliyoiomba kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia. “Mugalu amerejea nchini, lakini hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza dhidi ya Ihefu Jumapili hii, yeye yupo Dar akiisubiria timu itakaporejea. “Mshambuliaji huyo aliomba ruhusa maalum ya kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia ambayo tayari ameyamaliza,” alisema Sven.,


 MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Mkongomani, Chris Mugalu, tayari yupo nchini  baada ya kurudi kutoka nyumbani kwao DR Congo alipokwenda kumaliza matatizo ya kifamilia ila ataukosa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine.

Mugalu ni kati ya wachezaji wapya wa kimataifa waliosajiliwa na Simba katika kukiimarisha kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck.

 

Wengine ni Larry Bwalya, Bernard Morrison na Joash Onyango.Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Lusaka Dynamos inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia kumalizika.


Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven, amesema kuwa mshambuliaji huyo tayari ametua nchini baada ya kumaliza ruhusa ya wiki moja aliyoiomba kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia.

 

“Mugalu amerejea nchini, lakini hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza dhidi ya Ihefu Jumapili hii, yeye yupo Dar akiisubiria timu itakaporejea.

 

“Mshambuliaji huyo aliomba ruhusa maalum ya kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia ambayo tayari ameyamaliza,” alisema Sven.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *