Posted By Posted On

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA IHEFU FC, on September 4, 2020 at 5:00 am

 UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine.Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Simba na Ihefu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambayo itaanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6.Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu muhimu.”Maandalizi ya kikosi yapo sawa na kwetu sisi baada ya kumaliza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC ilikuwa ni ishara kwamba tayari tumeshaanza Vita kutafuta ushindi kwenye mechi zetu,”.Mchezo wa Ngao ya Jamii ulichezwa Agosti 30 kati ya Simba na Namungo FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.Simba ni mabingwa watetezi wameshaanza mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ikikutana na  Ihefu ambayo imetoka kupanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.,

 

UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu utakaopigwa Septemba 6, Uwanja wa Sokoine.


Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Simba na Ihefu ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 ambayo itaanza kutimua vumbi rasmi Septemba 6.


Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu muhimu.


“Maandalizi ya kikosi yapo sawa na kwetu sisi baada ya kumaliza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya Namungo FC ilikuwa ni ishara kwamba tayari tumeshaanza Vita kutafuta ushindi kwenye mechi zetu,”.


Mchezo wa Ngao ya Jamii ulichezwa Agosti 30 kati ya Simba na Namungo FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.


Simba ni mabingwa watetezi wameshaanza mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ikikutana na  Ihefu ambayo imetoka kupanda daraja kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *