Posted By Posted On

THIAGO AZIGOMEA KIMTINDO TIMU ZINAZOIWINDA SAINI YAKE, on September 4, 2020 at 9:02 am

 NYOTA anayekipiga ndani ya Klabu ya Bayern Munich ambao ni Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Thiago Alcantara amesema kuwa anapenda kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2020/21.Mchezaji huyo ambaye alikuwa kwenye kikosi kilichoichapa bao 1-0 PSG kwenye mchezo wa fainali alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Klabu za Manchester United na Liverpool ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.Thiago amesisitiza kuwa kwa sasa anafurahia maisha yake ndani ya Ujerumani wakiwa pia na taji la Bundesliga walilotwaa msimu wa 2019/20 na wanatumia Uwanja wa Allianz Arena kwenye mechi zao za nyumbani.Kiungo huyo amesema hayo muda mfupi baada ya timu yake ya Taifa ya Hispania kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Ujerumani jana kwenye mchezo wa kombe la mataifa.”Nina furaha kuwa ndani ya timu yangu kwa sasa na ninafikiria mchezo wetu dhidi ya Ukraine baada ya hapo labda nitajua mambo yatakuaje. Bayern ni nyumbani na ninafurahi kuwa pale,” amesema.,


 

NYOTA anayekipiga ndani ya Klabu ya Bayern Munich ambao ni Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Thiago Alcantara amesema kuwa anapenda kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2020/21.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa kwenye kikosi kilichoichapa bao 1-0 PSG kwenye mchezo wa fainali alikuwa anatajwa kuingia kwenye rada za Klabu za Manchester United na Liverpool ambazo zinashiriki Ligi Kuu England.

Thiago amesisitiza kuwa kwa sasa anafurahia maisha yake ndani ya Ujerumani wakiwa pia na taji la Bundesliga walilotwaa msimu wa 2019/20 na wanatumia Uwanja wa Allianz Arena kwenye mechi zao za nyumbani.

Kiungo huyo amesema hayo muda mfupi baada ya timu yake ya Taifa ya Hispania kumaliza dakika 90 kwa kufungana bao 1-1 na timu ya Taifa ya Ujerumani jana kwenye mchezo wa kombe la mataifa.


“Nina furaha kuwa ndani ya timu yangu kwa sasa na ninafikiria mchezo wetu dhidi ya Ukraine baada ya hapo labda nitajua mambo yatakuaje. Bayern ni nyumbani na ninafurahi kuwa pale,” amesema.


,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *