Posted By Posted On

YANGA IPO KAMILI GADO KUIVAA TANZANIA PRISONS, on September 4, 2020 at 6:00 am

 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa maandalizi yao kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons yapo vizuri.Yanga itakutana na Prisons, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6 majira ya saa 1:00 usiku ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2020/21.Akizungumza kuhusu hilo Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ushindani na wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu.”Wachezaji na benchi la ufundi kiujumla wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, tunajua utakuwa mchezo mgumu ila tunawaheshimu.”Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa kwa asilimia kubwa tumefanikisha maandalizi ya mwisho kwa umakini kabisa,” amesema Bumbuli.Yanga kwa sasa imeweka kambi  kwa ajili msimu wa 2020/21 Kigamboni.,

 

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa maandalizi yao kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons yapo vizuri.


Yanga itakutana na Prisons, Uwanja wa Mkapa, Septemba 6 majira ya saa 1:00 usiku ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2020/21.

Akizungumza kuhusu hilo Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ushindani na wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu.

“Wachezaji na benchi la ufundi kiujumla wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, tunajua utakuwa mchezo mgumu ila tunawaheshimu.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti kwa kuwa kwa asilimia kubwa tumefanikisha maandalizi ya mwisho kwa umakini kabisa,” amesema Bumbuli.

Yanga kwa sasa imeweka kambi  kwa ajili msimu wa 2020/21 Kigamboni.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *